godson Lomayani
JF-Expert Member
- Dec 31, 2018
- 538
- 711
Pambano hili limepigwa leo asubuhi katika jiji la New Jersey,hakika huyu binti wa Kimarekani Claressa Shields kutoka jimbo la Michigan ameonyesha uwezo mkubwa wa kusukuma makonde dhidi ya mpinzani wake Christina Hammer kutoka Dortmund,Ujerumani.Pambano lilikuwa la raundi kumi, japo mjerumani alijaribu kujitutumua katika raundi za mwanzo, lakini kibao kilimgeukia na kuanza kupigwa combination za uhakika kutoka kwa Claressa.Hadi mwisho wa mchezo Mmarekani aliibuka kidedea. Kiukweli nimefurahishwa na uwezo wa Claressa,anapiga punch za uhakika mithili ya Mayweather.Dada zetu wakiangalia mpambano huo unaweza kuwa inspire na kujikuta wakianza kujifunza Boxing.
Sent using Jamii Forums mobile app
Sent using Jamii Forums mobile app