Bozi: Wema Sepetu niachie Bob Junior wangu tafadhali

figganigga

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
25,724
Reaction score
55,906

Mwigizaji chipukizi katika tasnia ya filamu Bongo, 'Bozi' akihuzunika.

Jambo limezua jambo! Siku chache baada ya kuripotiwa kwa tukio la staa wa sinema za Kibongo, Wema Isaac Sepetu kunaswa kimalovee na Rais wa Masharobaro, Raheem Rummy Nanji ‘Bob Junior', mwigizaji chipukizi, Bozi ameibuka na kudai ‘Wema niachie Bob Junior wangu'.

Kwa mujibu wa chanzo chetu, mara baada ya habari hiyo kuruka hewani kupitia gazeti tumbo moja na hili, Amani la wiki iliyopita, mrembo huyo alipoziona picha za wawili hao alipoteza fahamu.
Akizungumza na Ijumaa Wikienda huku akiangua kilio, Bozi alisema kuwa katika siku alizowahi kuumia ni siku hiyo alipoona Wema ametoka kwenye gazeti na mpenzi wake huyo.



Staa wa sinema za Kibongo, Wema Isaac Sepetu akiwa mapajani mwa 'Bob Junior'.

Bozi alifunguka kwamba, alimbana Bob Junior kwa maswali lakini jamaa huyo hakutaka kumweka wazi kama yeye na Wema wanatoka.


Chanzo:GPL
 
Bob junior yupo na sabby angel sasa huyo bozi katokea wapi?
 
Ni kama wana invest katika kutengeneza iconic brand yao ili waje kuvuna mbele,coz huyo bozi wanamvika usupastaa wa lazima,sijawah hata kumwona!!
 
huyu naye n celebirty worth kuja kujadiliwa apa kweli? picha yenyewe amepiga nyumba cjui anakaa mabonden kuta zimeharibika za maji!!
 
Baada ya wema kutoka vichwani mwa watu kaamua kujianzishia habari boza nalo limepata pa kutokea. ila Bob juniur ndio nani?????????????
 
Hebu nielemisheni mie kijana wa zamani mshamba wa leo ,huyo Bozi ukitoa uhusiano wake wa kizinzi na watajwa hapo ni igizo lipi la kuonekana aliloshirikishwa! maana naona kila kukicha tunaletewa vinyago na kufanyiwa manyago!
 

Huo ni upumbavu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…