elmagnifico
JF-Expert Member
- Jul 7, 2011
- 8,260
- 9,764
Heheh hiyo bei makini ungemwaga specs zote sasa uwashawishi wadau, kwa specs ulizoweka wengine watashangaa maana hata zile lower end laptop za 600-500k wanaonaga specs hizo hizo,
Mkuu jana tu nimetoka kutoa 2.5M kwa XPS 14" core i5 4Gb ram. I wish ungekuwa umeliweka hili bandiko mapema.
Kaulizia bei xps yenye specifics hizo mkuu hii si kama zile dell na hp probook hii ni mahusus kwa wale wanaofanya mambo ya editing videos na graphics na mambo mengne ndo maana hata dsplay yake ni bora tofaut na nyngne
Mkuu nafahamu kwamba hyo mashine ni high end laptop na bei zake zimesimama nilichoshauri ni kumwaga specs nyingi kwasababu sote tunajua hizo mashine zina features nyingi sana, si unajua tena wabongo hawakawii kulalama.
Ila lengo langu kuu ilikuwa ni kuongeza details za hyo mashine mfano mdogo bila shaka hyo mashine ina GPU ya maana i.e Nvidia au AMD gpu hivi ndo vitu vinafanya bei zake kua juu na na specs nyinginezo nyingi ambazo hujataja. Ni hayo tu