Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,599
- 9,532
Rais wa Brazil Jair Bolsonaro ametia saini kanuni ambayo inakusudia kuzuia mamlaka za kampuni za mitandao ya kijamii kufuta akaunti na machapisho.
Kulingana na ripoti ya BBC, Bolsonaro alisema kuwa mabadiliko ya kanuni yanahitajika ili kupambana na kufutwa "kiholela" kwa akaunti za watumiaji.
Bolsonaro pia alisema kuwa kanuni mpya itasaidia kulinda uhuru wa kujieleza wa watumiaji.
Kanuni mpya inalenga kuleta uwazi kwa mamlaka za kampuni za mitandao ya kijamii kudhibiti maudhui.
Kanuni inahitaji wafanyabiashara wakubwa kutoa "sababu yenye msingi na chanzo" kabla ya kufuta akaunti au machapisho.
Wakati wa janga la virusi vya corona (Kovid-19), Twitter na Facebook zilifuta machapisho mengi yaliyoshirikiwa na Bolsonaro na wafuasi wake kwa kuchukuliwa kuwa ya kupotosha.
Mnamo Julai, YouTube iliondoa karibu video 15 kutoka kwa kituo kinachomilikiwa na Bolsonaro kwa madai ya kueneza habari potofu kuhusu Kovid-19.
Mwaka jana pia, Facebook ilitii uamuzi wa Korti Kuu kuzuia akaunti za wafuasi wengi wa Bolsonaro, ambao walituhumiwa kwa kuwasema majaji vibaya.
Bolsonaro tangu wakati huo amewaelekeza wafuasi wake kwa majukwaa mbadala kama Telegram na Parler.