Breaking new: Prof Mahalu ashinda kesi

Breaking new: Prof Mahalu ashinda kesi

Wikiliki

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2010
Posts
528
Reaction score
141
Wana jf prof. Mahalu ameshinda ile kesi yake iliyokuwa inamkabidhi mara baada ya kusoma leo.
 
Bwana Benjamin Mkapa alisema taratibu zilifatwa....na Kikwete ivo ivo ..Yaani ukiona Umefungwa na serikali hii ujue we Maskini wa mwisho

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 
Ningefurahi kama Kikwete angetinga mahakamani kutoa ushahidi wake, tujue alikuwa upande gani wa kumtetea Mahalu au wa kumpinga kwa kuwa yeye alikuwa balozi wa nchi za nje kipindi ambacho Mahalu alikuwa balozi Italy.
 
Bwana Benjamin Mkapa alisema taratibu zilifatwa....na Kikwete ivo ivo ..Yaani ukiona Umefungwa na serikali hii ujue we Maskini wa mwisho

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
Mkuu Kikwete alishasema?
 
Ama kweli hawa jamaa wanajua kuchezea akili zetu... Wamepoteza muda na hela za serikali kwa matokeo ya kipuuzi namna hii, hivi serikali haina wanasheria makini? Mbona inashindwa shindwa tu kizembe namna hii? Hivi kulikuwa na umuhimu gani wa kukomaa na hii kesi?
 
Walivyo na mambo ya ajabu watakata rufaa...
 
Mbwembwe za Rais Jk na pccb za kupereka watumiwa mahakamani zimeishia hapo
 
Ama kweli hawa jamaa wanajua kuchezea akili zetu... Wamepoteza muda na hela za serikali kwa matokeo ya kipuuzi namna hii, hivi serikali haina wanasheria makini? Mbona inashindwa shindwa tu kizembe namna hii? Hivi kulikuwa na umuhimu gani wa kukomaa na hii kesi?
Kumbe haki ya mtu ni upuuzi?
 
kiini macho tanzania. this kantryi bwana kwa kweli imelaaniwa
wezi wa kuku na vidagaa wanaozea selo lakini mapapa yanapeta tu.
 
Mbona wengine mnatoa hukumu zenu!? Inaonekana mlitaka Prof Mahalu ashindwe hata kama hana hatia?
Muacheni apumue jama!
Kwani serikali iliyompeleka mahakani c inaongozwa na walewale waliokuwepo kipindi hayo makosa yakifanyika? Wao wanaujua ukweli.
Kinachouma ni pesa zetu zilizotumika maana hata angepatikana na hatia angefungwa na c kurudisha hicho wanachodai amesababisha hasara (refer to Liyumba)
 
[h=3]Balozi Mahalu ashinda kesi[/h]
THURSDAY, AUGUST 09, 2012 FATHER KIDEVU NO COMMENTS
1.jpg
Balozi Profesa Mahalu akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kushinda kesi yake katika mahakama ya kisutu leo. PICHA NA FULLSHANGWEBLOG
4.jpg
Waandishi wa habari wakimfuata Balozi Profesa Mahalu akiwa pamoja na Mdogo wake Mirasi Rama wakitoka nje ya Mahakama ya Kisutu Mchana huu mara baada ya kushinda kesi iliyokuwa ikimkabili akidaiwa kununua nyumba ya Ubalozi wa Tanzania nchini Italia, Akisoma hukumu iliyosomwa kuanzia Saa sita leo na Hakimu Mfawidhi mkazi wa mahakama ya Kisutu Mh. Ilivin Mugeta imemtoa Balozi Profesa Mahalu katika hatia na kumwachia huru

2.jpg

Wakili wa Balozi Profesa Mahalu Bw. Alex Mgongolwa akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya mteja wake kushinda kesili iliyokuwa ikimkabili kwenye mahakama ya Kisutu jijini Dar es salaam.
3.jpg

Balozi Profesa Mahalu katikati akitoka nje ya mahaka ya Kisutu huku akiwa ameongozana na mdogo wake Mirasi Rama kulia ni Wakili wa kujitegemea Mabere Nyaucho Marando.

Posted in:
 
Kesi zote za ubadhilifu wa mali ya umma uwa ni danganya toto, ningeshangaa km angeshindwa kesi!
 
Ama kweli hawa jamaa wanajua kuchezea akili zetu... Wamepoteza muda na hela za serikali kwa matokeo ya kipuuzi namna hii, hivi serikali haina wanasheria makini? Mbona inashindwa shindwa tu kizembe namna hii? Hivi kulikuwa na umuhimu gani wa kukomaa na hii kesi?

Mkuu acha tu maana kinachofata atalipwa mabilioni kama fidia .
 
Wana jf prof. Mahalu ameshinda ile kesi yake iliyokuwa inamkabidhi mara baada ya kusoma leo.

Mazingaombwe yamekataa. Serikali ingeshinda ingesaidia sana kuonekana kama inayopinga dhuluma na ubadhirifu wa mali ya umma. Sijui kwa nini hawakujipanga ili kuhakikisha wanashinda. Hii ni serikali ya wasanii kweli kweli. Iliwezekanaje Raisi aliyepo madarakani amfungulie mashitaka mfanyakazi wake na Raisi aliyempokea aje kumtete? Hawakuwasiliana kuwa huyo hana hatia? Sasa huyu katoka na wengine wataendelea kutoka tu maana ki msingi si kweli kuwa serikali ina nia ya dhati ya kupambna na ufisadi. Ni mazingaombwe tu. Kazi tunayo.
 
Back
Top Bottom