Hapa hakuna chama chochote kinachohusika. Ni kero za muda mrefu sana. Walimu walitafakari kwa kina sana majaaliwa ya watoto wa kipangwa(kabila la hapa) na watoto wa A-level kutoka sehemu mbali2 za Tanzania ambao wanafeli sana wakati suluhisho lipo wazi. Tunalenga kuondoa uozo. Polisi wakivamia watakosea hii ni migomo ya amani.
Hivi ninavyoandika kuna migomo mizito miwili hapa shuleni Ulayasi wilayani Ludewa. Walimu wanamkataa msarifu wa shule(bursar) kutokana na ubadhirifu uliopitiliza. Wanafunzi wanadai kutimiziwa kero ambazo hazijaondolewa. Hivi tumeambiwa askari, mkuu wa wilaya na afisa elimu sekondari wanakuja toka makao makuu ya wilaya Ludewa. Walimu hawaingii darasani mpaka mkurugenzi amuondoe mhasibu. Ni mgomo usiyo na kikomo. Shule ina wanafunzi zaidi ya 1500 A-LEVEL na O-LEVEL. Source- mimi mwenyewe ni mwalimu hapa. We seek your help, congrats.
naomba niipost hii kwa blog
Halafu wewe mwalimu badala ushauri wanafunzi warudi madarasani wewe umekimbilia huku kwani bursar ndo mwalimu wa hao wanafunzi acheni kukuza mambo
Walimu wakigoma wataajiriwa wengine toka Malawi, na wanafunzi wataletwa wengine toka Msumbiji!
Poa ndugu, ni mtazamo wako tu!
Naona umekurupuka swahiba kajipange upya. Mbona taarifa za ajali ya meli zimejaa JF badala ya SUMATRA? Nini vision na mission of JF? Umeniuliza nimewashauri mara ngapi hao watoto kabla ya leo? Unajua madhila ya tathnia ya ualimu? If you are politician with naive approach please be informed we are not politicians and we dislike it but we stand for the pedagogy of the oppressed!