BREKI KUVUTA UPANDE MMOJA

teac kapex

JF-Expert Member
Joined
Jan 23, 2011
Posts
470
Reaction score
137
Wadau naomba kujua tatizo ninini, gari aina ya nissan vannete ukishika breki inavuta kushoto kiasi kwamba ukiwa na speed zaidi ya 80 inaweza kuanguka, nimejaribu kupuliza zile pipe za mafuta kuona kama zimeziba lkn ziko sawa nikabadilisha master sillinder ya breki lakin shida bado ipo, na zaidi ukikanyaga mara mbili au tatu haivuti, ukiishia moja inavuta na pia inakuwa ngumu sana, naomba ushauri wenu.
 
Mkuu kama umefanya bleeding huo upande unaovuta na tatizo bado lipo nadhani fanya adjustment uangalie tena.. Ahsante
 
Hapo ni lazma ufanye Break adjustment tena
 
Mkuu tatizo sio upande unao vuta nenda katengeneze upande mwingine ambao hauvuti ndio una matatizo. Yaani kama gari inavuta kushoto ina maana upande wenye shida ni wa kulia..je hiyo gari inatumia ABS?? na vipi historia ya marehem ipoje?? Gari ilianza gafla au kunamatengenezo yalifanywa ndio ikawa hivyo??

Kutoka kwenye master kwenda kwenye miguu zinatoka pipe ngapi?? Kila mguu na pipe yake ?? Au??. Hembu jibu maswali hayo machache ili kupata mwanga wa nn ushauriwe cha kufanya.


Hapo in short ina maana upande wa kulia gari haishiki brake au kama inashika basi ni kidogo sana na upande wa kushoto gari ndio inashika sana brake..
Sijui kama umenielewa hapo mkuu au kama ushawahi endesha trekta utakuwa umenielewa maana trekta inashika brake mguu mmoja mmoja so ukipiga wa kulia gari itaelekea kulia
 
Mkuu kama umefanya bleeding huo upande unaovuta na tatizo bado lipo nadhani fanya adjustment uangalie tena.. Ahsante
No hapana mkuu sio upande unao vuta bali unao vutwa ndio kwenye tatizo..hapo kama atatengeneza upande unaovuta wa kushoto basi apunguze adjust ili iwe sawa na ule upande unao vutwa..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…