Mtoa Taarifa
JF-Expert Member
- Sep 21, 2024
- 213
- 671
Ni wazi kuwa BRELA imefanya kazi kubwa katika kusaidia usajili wa majina ya biashara na kampuni hapa Tanzania, lakini changamoto ya mtandao wao kusumbua inazidi kukatisha tamaa wengi, hasa nyakati za jioni!
Wajasiriamali, wafanyabiashara, na wananchi kwa ujumla wanategemea huduma za mtandaoni ili kuokoa muda na gharama. Lakini inakatisha tamaa pale ambapo unakuta mtandao haupatikani au unakwamisha hatua muhimu wakati wa usajili.
Tunaelewa kuwa hakuna mfumo usioweza kuwa na changamoto, lakini BRELA mnapaswa kuweka juhudi za makusudi kuhakikisha mtandao wenu unafanya kazi kwa ufanisi muda wote, bila kujali saa. Mfumo wa mtandaoni usiokuwa imara sio tu kikwazo bali pia kinadhoofisha juhudi za kukuza uchumi kupitia sekta binafsi.
Tunatoa rai kwa BRELA:
1. Boresheni miundombinu ya TEHAMA ili kuepuka kusuasua kwa mfumo wenu.
2. Panua uwezo wa mtandao wenu ili kukidhi mahitaji ya watu wengi wakati mmoja, hasa nyakati za jioni.
3. Toeni maelezo ya wazi na mawasiliano ya mara kwa mara kwa wananchi kuhusu changamoto za kiufundi na hatua mnazochukua kuzitatua.
Ni wakati wa BRELA kuonesha kuwa kweli mnatambua umuhimu wa huduma zenu kwa maendeleo ya taifa letu. 🇹🇿