BRELA kufanya maboresho ya Mfumo wa Usajili kwa njia ya Mtandao (ORS) Disemba 20 mpaka 23, 2024

BRELA kufanya maboresho ya Mfumo wa Usajili kwa njia ya Mtandao (ORS) Disemba 20 mpaka 23, 2024

Cute Wife

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
1,906
Reaction score
5,000
Wakuu,

TAARIFA KWA UMMA

CHANGAMOTO ZA MFUMO WA USAJILI KWA NJIA YA MTANDAO (ORS)

Dar es Salaam-19 Desemba, 2024

Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) inapenda kuutaarifu umma na wadau wake kuwa inatarajia kufanya maboresho ya miundombinu ya mfumo wake wa usajili kwa njia ya mtandao (Online Registration System, ORS) kwa siku mbili (2) kuanzia tarehe 20 Desemba 2024 saa 12:00 jioni hadi tarehe 23 Desemba 2024 saa 1:30 asubuhi. Wakati wa maboresho hayo, baadhi ya nyakati za kukatika kwa Mfumo zinaweza kutokea. BRELA inaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaoweza kujitokeza kutokana na Maboresho hayo.

Imetolewa na;
Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma

brela.jpg

Pia soma:
 
Back
Top Bottom