Lycaon pictus
JF-Expert Member
- Jan 31, 2021
- 9,189
- 16,128
Kwanza ninaona ni jambo zuri kwa hegomony ya USA kwenye uchumi wa dunia kuwa challenged. Kama ambavyo dola ya Marekani ilivyoiangusha paundi ya Uingereza kama sarafu ya dunia, ndivyo inapaswa nayo kuanguka. Lakini safari hii itapendeza kupata mchanganyiko wa sarafu zenye nguvu. Matumizi ya dola kama sarafu ya dunia umekuwa wizi wa mchana kweupe uliofanyika kwa miaka mingi sana.
Sasa basi, dola hiyo kama sarafu ya dunia nguvu yake kubwa inatokana na kutumika kwenye biashara ya mafuta. Biashara kubwa kuliko zote duniani. Na nchi zinazoipinga US na ubabe wa dola ni wazalishaji wakubwa wa mafuta duniani. Katika nchi zinazoongoza kuzalisha mafuta duniani, Tano zimo ndani ya BRICS. Baada ya kuingia kwa UAE, IRAN na Saudi Arabia.
Duniani wazalishaji wakubwa kumi wa mafuta ni USA, Saudi Arabia, Russia, Canada, China, Iran, Iraq, UAE, Kuwait na Brazil. Hapo utaona nchi tano zipo tayari ndani ya BRICS. Je BRICS ni kama OPEC(umoja wa nchi zinazozalisha mafuta) mpya? Kwa kuwa na wazalishaji wakubwa wa mafuta, tunaweza kusema BRICS imeishika Marekani penyewe?