Brigedia Jenerali Mabena, wilayani hakuna matangazo ya mafunzo ya JKT uliyoyatangaza

Brigedia Jenerali Mabena, wilayani hakuna matangazo ya mafunzo ya JKT uliyoyatangaza

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Posts
6,137
Reaction score
17,908
Nazungumza nawe Brigedia Jenerali Hassan Mabena, Mkuu wa Tawi la Utawala-Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), juma lililopita ulitangaza kuhusu mafuzo ya kujitolea ya JKT kwa vijana wa kitanzania. Ukawataka watanzania wazalendo wajitokeze na kujiunga na mafunzo hayo.

Vijana wenye sifa zitakiwazo walikusikia, wako tayari. Tayari kujiunga na mafunzo ya kujitolea ya JKT. Wanamiminika kwenye wilaya zao ambapo ulisema ndiko kutakaporatibiwa zoezi hilo. Vijana, kwenye wilaya zao, wanajibiwa kuwa matangazo bado hayajafika huko.

Brigedia Mabena, tafadhali fanya jambo, vijana wako tayari kujiunga na mafunzo ya kizalendo na yenye upendo kwa nchi yao Tanzania. Matangazo yatolewe, wenye vigezo wachukuliwe.

Sensa si siasa!

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwa sasa Dodoma)
 
Nafasi zimeshajaa siku nyingi sana.Halafu uchaguzi mkuu unaokuja utaruhusu tena CCM kushika dola!😁😁😁
IKvCW.png
 
Back
Top Bottom