British Airways yapanga kuishtaki Uingereza kwa mpango wake wa karantini

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532

Mmiliki wa shirika la ndege la Uingereza la British Airways anatafakari kuifungulia mashtaka serikali ya Uingereza kuhusiana na mpango wake wa karantini.

Afisa mkuu mtendaji wa shirika hilo, Willie Walsh amesema sheria hiyo mpya itahujumu hatua ya shirika hilo kuanza tena safari zake mwezi Julai.

Sheria hiyo ya karantini inasema kuanzia Juni 8 watakaowasili Uingereza kutoka nchi za nje watalazimika kusalia nyumbani kwa siku kumi na nne.

Jambo hilo limewasababisha watu wasikate tikiti za ndege kwa ajili ya likizo, jambo ambalo linairudisha nyuma sekta hiyo ambayo tayari imeathirika pakubwa.

Walsh amekiambia kituo kimoja cha televisheni Uingereza kwamba serikali haikushauriana na sekta ya usafiri wa ndege kabla kufikia uamuzi huo na kwamba anatafakari na mawakili wake kuhusu kuchukua hatua.
Walsh amesema anatarajia mashirika mengine ya ndege yachukue hatua kama hizo
 
Mmiliki wa British Airways ni ‘International Airline Group’ (IAG) kampuni iliyosajiliwa Spain. For now BA is just a brand operating in UK lakini si mali ya UK.
 
Labda wawashawishi wakubali vyeti vya kupima kutoka nchi walizotoka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…