BRN na uchekeweshaji wa mishahara

the ultimatum

JF-Expert Member
Joined
Dec 16, 2012
Posts
403
Reaction score
116
Mwezi uliopita (Mwezi October) walimu wanaofanya kazi wilaya ya Mwanga, mkoani Kilimanjaro walichelewa kupata mishahara kwa wakati waliouzoea. Kwa kawaida huwa wanapata mshahara kati ya tarehe 25 na 26 ya kila mwezi lakini kwa mwezi huo waliukosa mpaka tarehe moja ya November.

Lakini mwezi huu yaonekana tatizo ni la nchi nzima. Takribani malalamiko ya wadau kutoka mikoa yote ni kuchelewa kwa mishahara kwa mwezi huu. Walimu wanalia njaa, serikali ipo kimya. Mishahara yenyewe haikidhi na bado haieleweki nyakati za kutoka kwake.

Huku waziri akisisitiza utekelezwaji wa mkakati wa matokeo makubwa sasa BRN, walimu kila kona wanalalamika juu ya stahiki zao. Serikali haijali tena shida za walimu.

Kwa staili hii hiyo BRN itatekelezwa mbinguni lakini siyo kwenye ardhi ya mtanzania, walimu hebu tuchukue hatua hii serikali naona ishaanza kutupanda kichwani.
 
Heading ni ucheleweshwaji sio uchekeweshaji naomba Mods wabadilishe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…