BRT inahujumu uchumi kwa makusudi

BRT inahujumu uchumi kwa makusudi

Msanii

Platinum Member
Joined
Jul 4, 2007
Posts
25,252
Reaction score
36,513
Sekta ya usafiri hasa wa abiria jijini Dar ilielekea kupata ufumbuzi baada ya Serikali kuwekeza kwenye mradi wa mabasi yaendayo kasi almaarufu Mwendokasi.

Kinachoendelea baada ya hapo ni kwa wasimamizi wa mradi huo kuuendesha kama kampuni za Kipemba. Yaani wanafanyabiashara wanapojisikia.

Ahsubuhi ni muda wa wasafiri kuwahi kwenye shughuli za kujenga uchumi lakini unaweza kukuta nuda huo gari zao nyingi zimepaki vituo vya fery, kariakoo na kimara hayapakii bali wameweka tangazo out of service, na unayakuta mengine barabarani hayajabeba abiria yanakimbizwa kasi kutoka kimara hadi Kariakoo au fery yakiwa out of service.

Unaweza kukata tiketi ukasubiri gari kituoni hata saa nzima.

Watendaji wengi wa serikali huwa hawana uchungu na mali ya umma hasa kweye hizi kampuni za umma. Ukiangalia Tanesco Dawasco, Ewura na kadhalika mwendo ni ule ule.

Ninaamini endapo miradi hii ikisimamiwa vizuri, Serikali isingefikia hatua ya kukamua ng'ombe dume atoe maziwa kwa mfumo wa Tozo la Miamala....
 
Tatizo linakuja pale watendaji wote wakuu wa serikali na hata hao wanaosimamia mradi huu hawatumii mabasi haya, nafikri ili mradi huu uweze fanikiwa na kukidhi maana halisi ya kuanzishwa kwake kuna haja ya watendaji wakuu wa serikali waliopo Dar es Salaam na ambao wanaishi katika maeneo ambayo mradi huu unapita wakalazimishwa kutumia usafiri huu na kupaki magari ya serikali, vinginevyo tutaendelea kuona maajabu katika mradi huu pendwa!
 
Tatizo linakuja pale watendaji wote wakuu wa serikali na hata hao wanaosimamia mradi huu hawatumii mabasi haya, nafikri ili mradi huu uweze fanikiwa na kukidhi maana halisi ya kuanzishwa kwake kuna haja ya watendaji wakuu wa serikali waliopo dar es salaam na ambao wanaishi katika maeneo ambayo mradi huu unapita wakalazimishwa kutumia usafiri huu na kupaki magari ya serikali, vinginevyo tutaendelea kuona maajabu katika mradi huu pendwa!
Neno kubwa hili.

Ni kama ilivyo kwenye elimu pia
 
Serikali wangelimpatia mtu binafsi na wao wangelibaki kuchukua kodi tu
 
Wanatulazimisha kuvaa barakoa halafu wanatujaza Kwenye mabasi kama maharage kwenye gunia

Mwendokasi ni jipu lililoshindikana
Inawezekana ni miradi ya wakubwa kutupiga
 
Tatizo linakuja pale watendaji wote wakuu wa serikali na hata hao wanaosimamia mradi huu hawatumii mabasi haya, nafikri ili mradi huu uweze fanikiwa na kukidhi maana halisi ya kuanzishwa kwake kuna haja ya watendaji wakuu wa serikali waliopo Dar es Salaam na ambao wanaishi katika maeneo ambayo mradi huu unapita wakalazimishwa kutumia usafiri huu na kupaki magari ya serikali, vinginevyo tutaendelea kuona maajabu katika mradi huu pendwa!
Correct. Kitanda ambacho hujakilalia huwezi kujua kunguni wake. Hawa jamaa wanaosimamia mradi huu hawana uchungu na huu usafiri kwa kuwa hawatumii kwenda kazini kila siku. Hawajui madhara ya kucheleweshwa kazini kwa sababu ya uzembe wa watu wachache
 
Katika hao watu binafsi nawe una unavigezo vya kupewa huo mradi. Binafsi kitu ambacho sina vigezo navyo naona bora viendeshwe na serikali tu.

Kwa kuwa huna vigezo inamaanisha hakuna wengine wenye vigezo?
 
Out of service ina maana mabasi mabovu au wamechoka kazi ?

Ushauri BRT inatakiwa kubinafsishwa serekali iwe na hisa 51% mwekezaji awe na 49% na aachiwe kuendesha shughuli zote kwa uangalizi maalumu wa serekali .
 
Back
Top Bottom