Bruno Fernandez amefunga goli 18 na assist 33 chini ya mtaalam Ole Gunnar Solskjaer

marcoveratti

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2017
Posts
1,019
Reaction score
1,824
Bruno Fernandes sasa amehusika moja kwa moja kwenye magoli 23 katika mechi 21 za Ligi Kuu, wastani wa goli kila dakika 76.6

Katika mashindano yote, amefunga goli 18 na kutoa assist 13 katika mechi 33 kwa chini ya mtaalam Ole Gunnar Solskjaer.

Ana assist 10 za Ligi Kuu tangu mechi yake ya kwanza, zaidi ya kiungo yeyote wa EPL.

Tangu Fernandes alipocheza mechi ya kwamza Februari 2020, Mohamed Salah peke yake ndio mchezaji ndio anamzidi magoli na anagoli zaidi ya 13 kwa EPL.

Licha ya ukawa kumuita mzee wa penati, Bruno amefunga goli saba(7) ya ligi yasio ya penati tangu aje Manchester. Hakuna kiungo aliyefunga zaidi katika kipindi hicho sio De Bruine sio nani!

Akiwa na mabao 10 na assist 5, Fernandes anahusika kwenye goli nyingi kwenye mechi zake 10 za kwanza za EPL.

Hiyo ni idadi kubwa kuliko mchezaji yeyote katika historia ya mashindano hayo yani hakuna mchezaji alie husika kwenye hyo idadi ya magoli kwenye mechi zake 10 za kwanza EPL,kuanzia ma striker mpaka makipa hakuna.

Mbungi yake dhidi ya Everton ilimpa tuzo ya Man of match likua mara ya 5 Fernandes amepewa tuzo hyo toka kahamia England. Hakuna mchezaji aliyepokea zaidi yake tangu aje.

Bila kusahau kwenye picha huyo bwana ndio mchezaji alie tengeneza nafasi nyingi zaidi msimu huu 20,Kelvin De bruine anafatia ana 18

Bruno Fernandez ni mchezaji Bora EPL.

UKIBISHA UWE NA FACT NA STATISTICS

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…