Master J amewakosea watanzania kwa kuwatukana na kuwaita eti ni WASHAMBA kwa kuwa aliona watu wanamshangilia sana mzungu Joseph Payne kuliko wengine.
Kama kawaida yake Master J huwa hajiamini na kuwa miaka yote hatimaye anafuatisha kile anachotaka Salama Jabir.
Salama alisema toka mwanzo kuwa hayupo kwenye boti wala basi la mzungu, na hatimaye Master J kama kawaida yake akamuiga.
Walimkandia sana mzungu siku ile ya mwisho ili kumkatisha tamaa, wakati alifanya vizuri.
BSS imekuwa ni usanii mtupu sasa, wanapanga mshindi, na wasiowataka wanawahujumu.
Kwaheri BSS, hatutaonana tena; na karibu TPF (Tusker Project fame)