BSS msimu huu majaji wana kazi ngumu sana

Sasa ungeachaje kutokufuatilia mkuu... Mimi huwa naikumbuka hiyo BSS ya kina Walter kwasababu ilikuwa kwenye mwaka ambao matokeo ya kidato cha nne yalitoka, yakafutwa halafu yakatolewa tenaπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
Yale matokeo yaliumiza wengi sana Kuna ndugu yangu awamu ya kwanza alifaulu vizuri yalivyorudiwa akafeli
 
Wape kwanza vya zamani ili wajue kipi kipya wakuambie..!!!! Acha tabia ya kitu usichokipenda wewe basi kila mtu asikipende..!!
Hakuna mahali nimeonesha kuichukia hiyo BSS, nimeuliza tu, maana ya kitambo sana, zama za muziki na vyombo vya habari zimebadilika mnoo.
Mara ya mwisho kuifuatilia nimesema ni kama miaka 15 iliyopita (mwenye majibu ya kipi kipya) ataanzia kujua ni wapi niliisha.
Nimehoji kujua kama kuna mtu anaifuatilia, maana sioni vibe mitaani au kwenye media kuizungumzia.
 
Kumbe bado ipo!! Kitambo sana, ya mwisho kufuatilia ni ile ya akiba Walter Chilambo. Eti hadi kura nilimpigiagaπŸ™†β€β™‚οΈπŸ™†β€β™‚οΈ

Inaonyeshwa wapi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…