Jamani wanajukwaa la elimu nimesikia kuwa wanachuo wa ngazi ya cheti na ngazi ya stashahada mwaka wa pili wiki ijao watakuwa na BTP ya siku 14 lakini nashangaa posho zao zinatofautiana kila chuo.
Baadhi ya vyuo wameambiwa watapewa sh.2500/= kwa siku wakati vingine sh.3500/=
Sasa swali hivi wizara imetoa posho kulingana na idadi ya kila chuo au imetoa kwa ujumla wake , na je nikawaida mwanachuo kwenda BTP kwa siku 14 au la ?
Naombeni ushauri wenu wadau wa elimu.