Samahani kwa kutoka nje ya mada kidogo,kuna bubu alikuwa anachimba kisima katika shule moja,kisima hicho kilitakiwa kuwa na urefu wa takriban futi 40 basi wanafunzi wakawa wanamtupia ndoo kisha anajaza mawe yaliyochanganyika na udongo kisha wanayavuta na kumwaga juu.Basi mwanafunzi mmoja alikuwa na swali kama lako akitaka kujua bubu analiaje,basi alichokifanya ni kumwaga mchanganyiko ule wa mawe na kokoto jirani na shimo la kisima kisha vyote hivyo vikarudi ndani ya shimo na kumbonda yule bubu,kilichofuatia kilikuwa ni kilio kinachofanana na mlio wa farasi aliyechoka.