"Buffalo Hump" inatibika?

"Buffalo Hump" inatibika?

Head prefect

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2013
Posts
225
Reaction score
106
Habarini wakuu? Naombeni msaada wa kitabibu kwa yeyote aliyewahi kuwa na tatizo hili akalitatua au tabibu yeyote mwenye ufumbuzi wa tatizo langu.

Nimepata tatizo la uvimbe mgongoni nyuma ya mabega (upper back) mfano wa layer ya mafuta ambayo mwanzo sikuwa nayo. Uvimbe huu umekuwa ni kama mtu mwenye kibiongo, but ni pande la nyama linaloshikika na linaonekana lina mipaka (halijasambaa) sehemu kubwa. Nimejaribu kuwauliza baadhi ya madaktari kwenye hospitali kama tatu hivi, wamenihoji kama natumia dawa za ARV nikamwambia hapana situmii. Wamenihoji kama nina HIV nikamwambia hapana.

Kiuhalisia sina HIV, na sina uzito mkubwa wa kutisha. Hili tatizo nilianza kulihisi baada ya kuwa napata maumivu mgongoni upande wa bega la kushoto, na huwa yanatokea nikifanya kazi ya kukaa ofisini kwa muda mrefu, Kila nikijaribu kujinyoosha na kushika eneo ambalo ni center ya maumivu ndipo nilipogundua kuwa na fat layer ya mafuta ambayo hata baadhi ya watu wa karibu walianza kunihoji kuwa ni kitu gani hicho.

Wakuu, kwa sasa bado hii fat layer inakua kiasi kwamba ku bend shingo kwa nyuma inanishinda sasa. Nimepita mitandaoni sijaona tiba ya moja kwa moja zaidi ya kitu wanaita cosmetic surgery. Wakuu naombeni kama kuna msaada wa tofauti wa kupambana na hii hali.

Nategemea msaada wenu wakuu
 
mkuu anza kwanza hospitali vipimo vikathibitishe ni nini hicho, usije kuwa unasema ni kama mafuta kumbe ndani ni kitu tofauti na hujui kimeanzia wapi kwa ndani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom