Buffon: Messi Amekamilika zaidi kuliko ‘Muuaji’ Ronaldo

Buffon: Messi Amekamilika zaidi kuliko ‘Muuaji’ Ronaldo

britanicca

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2015
Posts
16,295
Reaction score
33,994
:
NAHODHA wa Juventus Gianluigi Buffon,ameweza kumuelezea nyoto wa Barcelona Lionel Messi, kwamba ni mchezaji aliyekamilika kiufundi zaidi kuliko ‘muuaji’ Cristiano Ronaldo wa Real Madrid.

Hakuna mambo mengi ya kutofautisha kwa washindi hawa wa mara tano wa Ballon D'orz

Buffon alijaribu kumzungumzia Messi kabla ya mchezo wa kirafiki wa kimataifa utakaopigwa leo kati ya Argentina dhidi ya Italia, katika uwanja wa Etihad.

"Wao ni wachezaji wawili tofauti kabisa. Messi amekamilika zaidi kiufundi, kwasababu anaanzia nyuma zaidi, ana ubora wa kiufundi zaidi, na anaweza maono ya mchezo na anaweza kuchezesha timu.

"Ronaldo, pengine kwa sababu ya umri wake - hivi sasa amekuwa ‘muuaji’ zaidi kwenye eneo la penati. Labda kutokana na umri wake siku hizi amekuwa sio Ronaldo yule ambaye ungemkuta pembezoni mwa uwanja anakimbizana na mabeki na kujaribu kuwafanya anavyotaka - siku hizi anaifadhi nguvu zake na kufanya kazi yake kwenye eneo la hatari la wapinzani.”

FB_IMG_1521801238753.jpg
 
Kwani fainali ya Uefa champions league mwaka jana ilikuaje hivi Cr7 alimfunga kwa penalty eeh??
 
Mbona linajulikana hilo! Na sio cr7 tu, binafc sijaona mchezaji yeyote anaemzidi lapulga.
 
  • Thanks
Reactions: PNC
Back
Top Bottom