DOKEZO Bugando Hospitali mjitafakari wagonjwa kufia mikononi mwenu

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Hii hospitali sitamani hata kuisikia, ni mojawapo ya hospitali za Rufaa za ovyo kuwahi kuwepo nchini. Unampeleka mgnjwa yuko mahututi wanamweka emegency ndo biashara inaishia hapo. Mtu anafanyiwa CT-Scan unaambiwa unapaswa kusubiri majibu ya CT-Scan siku saba
 
Wanakuelewa basi?? Watu wetu wanahitaji sana elimu.. kwa uchanga wa akili zao wengi bado wanapenda Ile mihemko ya awamu ya tano
 
Kama ni mtumishi unakuja kusafisha njia hapa, bora ukae kimya, halijakukuta ndio maana una Bwabwaja kipuuzi hivi
 
Bugando ni moja ya hospitali Bora Sana kwa mazingira ya Tanzania... Mapungufu yapo Ila tusilaumu tu.. Kwanza kumbuka wagonjwa wengi wanaopelekwa hizo hospital za rufaa huwa wapo terminally ill... Yaani hatua ya mwisho kabisa ya magonjwa baada ya kushindikana kwenye hospitali za chini. Licha ya Hilo lakini wagonjwa wengi Sana hapo huwa wanapona au kupata nafuu na kuruhusiwa. Wengine hufariki ndio Ila sio kila Mara ni uzembe.

Naifahamu vizuri sana hiyo hospitali kwasababu nilisoma hapo, kwakweli wanajitahidi, wagonjwa ni wengi Sana kutoka kila sehemu ya Kanda ya ziwa na baadhi hutoka Uganda huko. Changamoto zipo Ila isiwe Sababu ya kuibeza hospitali iliyosaidia watu wengi Sana.
 
Kama unaangalia Mazingira hongera, ila mimi kilichomkuta mdogo wangu na Mungu amuweke mahala pema peponi ukinambia hiyo hospitali ina Mazingira mazuri labda kama unaangalia majengo. Kwa kifupi mimi mdogo aliteseka pale mpaka nikataka kuchanganyikwa.Na kama ulkuwa unasoma basi hupaswi kutoa hoja kuhusiana na huduma kwa sababu wewe ni sehemu ya walalamikiwa. Imagine kipimo tu cha CT-Scan unaambiwa majibu mpaka siku saba? CT-Scan siku saba alafu wakati huo mtu yuko emergency ward bila matibabu yoyote. Mpaka tuliamua kumtoa mgonjwa hosptali na kumrudisha akajifiye nyumbani. Alafu wasivokuwa na aibu baada mdogo kufariki ndo napigiwa simu eti kama unaweza mrudishe mgonjwa hospitali ili turudie kipimo baada ya kuchomwa dawa ili tuweze kuona vizuri. ALAFU mnakuja kuimba mapambio kuwa ni Hospitali Bora, Hebu njoo Mloganzila, Tumbi na Mhimbili uone huduma za matibabu zinavyotelewa. Umesikia mtu akilalamika kuhusu Mloganzila, Tumbi na Mhimbili? Lakini Bugando unapesa yote inayohitajika kulipia huduma bila kuwaonga madaktari utasubiri sana. Na walivowaajabu kama uko mbali na kuomba uongee nao kwa simu hawakubali kabisa. ENDELEA KUSIFIA siku likikuta utararudi kuungana na sisi
 
Kwanz
Kwanza pole ndugu, naelewa upo dissapointed Sana.. Na una haki ya kulalamika. Pili, sijasifia nimesema mapungufu yapo Ila nimeelezea hali ya hospitali pia Ina wagonjwa wengi sana.

Kuhusu CT Scan kwakweli sijawahi kuona mtu anaambiwa asubiri siku saba... Mara nyingi huwa ni siku moja tu mtu anapewa majibu. Siwezi kuhukumu moja kwa moja, Ila nachoweza kusema kunahitajika maboresho Kama Kuongeza Staff na vifaa... Kumbuka hospitali inahudumia mikoa zaidi ya tano na inamilikiwa na kanisa.

Huko Muhimbili na Mloganzila napafahamu pia wako vizuri zaidi kwa sababu serikali imewekeza sana huko... Ukilinganisha na BMC... Lakini hata wao Wana changamoto zao.
 
Bei yao sasa hatari haijalishi umekufa au umepona

Afu na utaratibu wao wa mgonjwa kulala peke yake wodini eti wanamwangalia wakat hata muda huo hawana,wengi wanakufa kwa kukosa uangaliz wa karibu
 
True. Ila kwa maoni yangu waziri wa afya yafaa awe Daktari, waziri wa sheria yafaa awe mwanasheria.

Tz waziri wa sheria mara kadhaa sio mwanasheria unajiuliza why?
Sio kweli. Na hiyo ni dhana potofu kwa Wabongo. Dr. Ben Carson ambaye ni Daktari Bingwa Marekani aliwahi kuteuliwa na Donald Trump kuwa Waziri wa Makazi.
 
Nikiri wazi kuwa Bugando imekuwa taasisi ya fedha sio hospital...
Huduma mbovu sana na madaktari wanafanya 'trial n error' kwenye mwili wa mtu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…