Bugando wanaleta mzaha kwenye afya za wa Wagonjwa wa Figo. Dr. Gwajima fuatilia hili

Bugando wanaleta mzaha kwenye afya za wa Wagonjwa wa Figo. Dr. Gwajima fuatilia hili

Ta Muganyizi

R I P
Joined
Oct 19, 2010
Posts
5,355
Reaction score
2,736
Imekuwa mazoea sasa ambapo watu wanaopata huduma ya Dialysis pale Bugando kushindwa kufanyiwa huduma kwa kuambiwa kuwa vifaa havipo au havijafika.

Wagonjwa wa Dialysis idadi yao inajulikana na forecast inafanywa kwa kujua mahitaji lakini inafikia sehemu wagonjwa mpaka wanalala kwenye chumba cha dialysis usiku mzima wakisubiri vifaa. Huu ni uzembe wa hali ya juu.

Hatujui kama Mkurigenzi wa hospitali ana taarifa na inawezekana kuna mtumishi mmoja kwa matakwa yake anakwamisha zoezi. Kama mhasibu anawalipa wazabuni wanaoleta mzigo inakuwaje tatizo linatokea mara kwa mara.

Siku ya Ijunaa watu wamekaa kwenye chumba cha Dialysis kunazia saa 4 usiku mpaka asubuhi vifaa havijafika. Wauguzi walikuwepo na wana nia nzuri ya kuwasaidia wagonjwa na ukiwauliza kuhusu vifaa wanasema iko nje ya uwezo wao na ni kweli.

Tumuombe mkurugenzi wa Bugando asikubali mtu mmoja au wawili waharibu sifa ya Bugando. Wafuatilie watu wako inakuwaje vifaa vinakosekana. Kuthibitisha haya njoo uwahoji wagonjwa wa Dialysis watakueleza shida zao.

Kutokana na kukosekana huduma siku ya Ijumaa usiku mmoja wa Wagonjwa mpaka sasa imebidi alazwe baada ya maji kujaa kifuani na mpaka sasa yuko Wodini. Kama anayehusika na manunuzi ya vifaa hajui umuhimu wa dialysis basi aelimishwe ajue kwamba anacheza na maisha ya watu.

Hope Mama Dr. Gwajima atatoa maelekezo kwa hili.
 
Pole mkuu, nilikua na mgonjwa anajaa maji kifuani. Muhimbili walicheki wakashindwa kupata tatizo ikabidi watoe maji kwanza. Baada ya kupungua bado hawakuona ikabidi nimpeleke private kakutwa na TB na dozi aendelea nayo.

Usihofu mgonjwa wako atakua sawa
 
Back
Top Bottom