Buguruni kunalemaza sana wakuu, hebu angalia nguvu ya 500!

Buguruni kunalemaza sana wakuu, hebu angalia nguvu ya 500!

aise

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2018
Posts
5,175
Reaction score
16,488
Hii ni Supu ya shilingi 500 hapa Buguruni, hivi kwa hali hii unaweza ukapata akili ya kuwa na vitu vikubwa? Buguruni hii kuna mpaka Chips za 500.

Wali ule unaouzwa 2,000 maeneo mengine hapa tunauziwa 1000, kuna mpaka kipimo cha 500 kama ukiomba unapata wali na maharage.

Nataka nihame hapa Buguruni maana tangia nimehamia hapa ni kama nimepunguza kasi ya kupambana.

20240505_090432.jpg
 
Hii ni Supu ya shilingi 500 hapa buguruni, hivi kwa hali hii unaweza ukapata akili ya kuwa na vitu vikubwa?
Buguruni hii kuna mpaka Chips za 500,
Wali ule unaouzwa 2000 maeneo mengine hapa tunauziwa 1000, kuna mpaka kipimo cha 500 kama ukiomba unapata wali na maharage!
Nataka nihame hapa Buguruni maana tangia nimehamia hapa ni kama nimepunguza kasi ya kupambana!
View attachment 2982368
Hiyo mixer unaweza kuta ni ya ng'ombe kama 10 hivi.
 
Mkuu,

Kuwa makini na supu za buguruni, pamoja na nyama ya mbuzi ambayo huoni kichwa wala mkia wa mbuzi.

Ile unauliza nyama Gani unajibiwa tu, hii ni nyama ya mbuzi!! Utakula nyama zisizoeleweka kutoka vingunguti hapo.

Ng'ombe washajifia hawaachwi Bure Bure.
 
Nyama robo ni 2500 na inatoa vipande 18 vidogo vidogo yva nyama. Hii wanauza 500 Ina vipande vingi hivyo wanatoaga wapi? 🤷🏿‍♂️🤷🏿‍♂️🤷🏿‍♂️🤷🏿‍♂️🤷🏿‍♂️
 
Back
Top Bottom