Bukavu: M23 yakaribia uwanja wa ndege wa Kavumu

MBOKA NA NGAI

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2025
Posts
350
Reaction score
576
Baada ya Goma kuangukia mikononi mwa M23, mtutu wa bunduki ulielekezwa Kivu kusini, huku mji mkuu ukiwa Bukavu.

Serikali ya Burundi kwa makubaliano na DRC, ilipeleka wanajeshi wapatao elfu 10 kuhakikisha Bukavu inalindwa kwa nguvu yote.

Uwanja wa Kavumu, unatumiwa na serikali ya Burundi na DRC kuleta siraha toka Kinshasa na Bujumbula.

Baada ya wanajeshi hao kushindwa kuwazuia wakiwa Kalehe, vita vinaendelea eneo la Katana, ambalo lipo umbali wa km 11 tu kutoka uwanja wa ndege huo wa Kavumu.

Kukamatwa kwa uwanja huo, kutaondoa uwezekano wa serikali ya Burundi na kinshasa kuongeza nguvu. Hapo juzi, jeshi la Congo lilivamia wafanyabiashara na kupora mali zao, benki zimeibiwa.

View: https://x.com/kabagambei/status/1888701569870319802?s=46
Video, ni wanaouwawa Kivu kusini,kisa kuwa watutsi.
 
Wanajeshi elfu 10??? Something fishy
 
Mungu wabariki wapigania haki wa M23, na uliangamize jeshi la wanyang'anyi la serekali ya congo pamoja na majeshi ya nchi jirani yaliyoenda kuwasaidia
 
Kwa namna nilivyojua chanzo Cha mgogoro ni kubaguliwa Kwa banyamulenge ambao walitenganishwa na mipaka tu ya kikoloni na hitimisha Kwa kuwatakia M23 ushindi mnono ili kuuondoa huo ubaguzi wa kijinga wa watawala wa DRC.yaano ni sawa na sisi tuseme wamasai siyo watanzania Kwa sababu Kuna wamasai wanaoishi Kenya.
 
Hamna jeshi kabisa...

Ila mkusanyiko wa wanamgambo..
Hawana hata hadhi ya kuitwa wana mgambo bali ni kikundi cha panya road .

Maana hiyo m23 inayo waenyesha ni wana mgambo ,hamas ni wana mgambo lakini spirit yao ya kupamba kila mtu kaiona, Hizbulla,huthi wote ni wanamgambo lakini shughuli yao ni pevu yaani sijui jeshi la kongo tulifananishe na nn.
 
Back
Top Bottom