Bukavu: maandalizi ya kujihami yaendelea

MBOKA NA NGAI

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2025
Posts
350
Reaction score
576
Kama kawaida, habari ziwafikie wote mnaopenda vita(roho za wenzenu zipo juu, wengine wanakula kama hakuna kinachoendelea)

Toka jana, badhi ya maeneo mengi ya Bukavu, wanaonekana wanajeshi wa M23. Wamekaribishwa kwa shangwe,
Tangazo la kukomboa mji wa Bukavu halijatolewa. Chanzo nini? Tulia nikuhabarishe.

Baada ya hiyo jana jeshi la Burundi na Afrika kusini kunyang'anywa uwanja wa ndege wa Kavumu, jeshi la Burundi lilikimbia uelekeo wa Uvira. Mpaka sasa, inasemekana wanasubiliwa wanajeshi wa Afrika kusini na Burundi kuongeza nguvu, ili waikabili M23 ifukuzwe katika maeneo yote inayochunga kwa sasa.

M23 kwa upande wao pia, kila aina ya taarifa wanayo, na ndo maana hawataka kuingia mazima mjini au kutangaza chochote. Huenda na wenyewe wanajiandaa kucheza sebene hilo.

Ikumbukwe, baada ya South Africa kuipeleka Israel mahakama ya kimataifa ikishitakiwa mauaji halaiki huko Palestina, huyo ni adui wa msaouth aliejipatia njia nyepesi ya kumuweka kwenye kaangio.

Kila kinachojili, mtajuzwa tuu
 
Sawa waache waendelee kuumizana sisi huku tunajenga nchi...
 
Hivi m23 imeshindikana kweli,jeshi la congo linafanya kazi gani kushindwa kukiondoa hicho kikundi
 
-Wanakiondoa kukipeleka wapi? Jiulize kwanza kina faida gani kwenye vita hivyo.
-Congo haina jeshi, ina genge la wahuni. Wakubwa wanakula meza moja na ma Boss, wadogo wanawapora raia mari zao na kubaka wanawake.
Hilo jeshi limerecruit wazalendo wengi, japo karibia wote marehemu. Jiulize vijana wadogo wadogo ambao ndo wangekuwa taifa la kesho,umewaweka front wameuliwa, unabaki na wazee wa miaka 70 jeshini. Af unajiona una jeshi. Hamna kitu.
M23 ilishajipanga na kama ina wafadhili,wako vizuri walishafanya assesment na kuanza wakiwa na uhakika wa kutoboa.
Wameleta majeshi mangapi yaliyoshindwa? Uachane na porojo za mtandaoni kwamba ingekuwa hivi na vile! Ktakachotokea na vioongozi kupishana kauli na mtu mmoja ataenda ziara kikazi na hatorudi.
 
Hii ni point kubwa ya South na Rwanda ndo kubwa kuliko
 
Nikiangalia picha za wanajeshi wa FARD huwa najiuliz mbona wengi km sio wote waana mionekano ya kiutuuzima sana 40 to 60 na sura za pombe?!kumbe hii ndio sababu,asante mkuu
 
Hivi m23 imeshindikana kweli,jeshi la congo linafanya kazi gani kushindwa kukiondoa hicho kikundi
Congo Hawana jeshi...ajira zao ni za kubebana tu...ni jeshi lisilo na nidhamu...Makamanda wao ni hovyo na wasaliti...uliwahi kuona wapi kama siyo Congo pekee ambapo Askari anaenda likizo na bunduki baadala ya kurudisha armoury?! Congo is a failed state...hakuna kitu pale...wanaume wamejaa misifa na kujichubua tu...nenda kinondoni Dar na Sinza utawakuta wakongoma I walivyo wajinga...mikongomani imejaa kwenye saloon za kike na kusambaza umbeya tu...stupid people.
 
Sawa waache waendelee kuumizana sisi huku tunajenga nchi...
Hawa kina mwigulu na makamba wanaoununua software India ya billion 70 Kwa ajili ya upeana taarifa tu ndani ya tanesco wakati simu zipo mpaka Leo haijulikani Nini kinaendelea
 
Nikiangalia picha za wanajeshi wa FARD huwa najiuliz mbona wengi km sio wote waana mionekano ya kiutuuzima sana 40 to 60 na sura za pombe?!kumbe hii ndio sababu,asante mkuu
Tukiweka ushabiki pembeni, hawana wanajeshi. Na hao hao, ndo wanaolipwa dolla 150. Kijana anayefanya kazi machimboni, anaingiza zaidi ya elfu moja. Mtu huyo,ana bunduki. Unategemea nini? Congo siyo kubwa kuliko nchi nyingine kubwa duniani. Mbona zinaongozeka! Tatizo uongozi. Kundi la watu wanajijali wenyewe,wale wao, wastarehe wao, matokeo ndo haya.
Hapo ongezea: vijana wadogo ndo wamepelekwa kupigana, wengi wameuwawa. Hao mabibi na mababu ambao hawastafu ndo watalinda taifa lao? Wenye nguvu hao, wangepewa mafunzo na kuwajali.

We angalia tu kila inapokanyaga M23, utagundua kuna kitu. Hata kama huwapendi, lakini utaona wana tofauti na jeshi la serikali,kwa ukalimu. Japo lazima wawe wakalimu,kuweza kuwin miyoyo ya wananchi. Hawa huwezi kuonewa wakiwepo. Lakini jeshi la FARDC nani anahangaika na wewe!
 
Zamani nilikuwa siwapend M23 hasa kipindi kile cha tensio ya Rwanda na Tanzania,ila kwa sasa ninapozidi kugundua nini chanzo cha mgogoro huu naanza kuwapenda M23 na kujua kwamba wacongo wana shida hasa baada ya kujua hapa chanzo cha yote haya ni ubaguzi wa wacongo kwa hawa Banyamulenge..Hata tukisema tuachane na zile notion sijui wanaungwa mkono na Kagame,sijui USA sijui mbelgiji lakini tukubali tukatae suala la ubaguzi huko mashariki dhidi ya Banyamulenge ndio chanzo cha haya yote,kagame asingetia pua kama wangekuwa ni wamoja
 
Badala ya kupigana Waafrika kwanini tusiungane?
 
Badhi ya viongozi wenye tamaa na vibaraka wa wazungu, hawawezi kuruhusu huo muungano. Kuna watu wao mpe pesa tu, hata raia wake ukitaka chukua tu. Yeye ale,ashibe na asaze, lakini raia wafe njaa, anaona kawaida tu. Huyo ataanzaje kujishusha thamani na kukubali muungano?
 
Back
Top Bottom