Bukoba: Kesi ya Mauaji ya Mtoto mwenye Ualbino (Asimwe) yahirishwa, kutokana na mshtakiwa kupelekwa Isanga

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Mahakama Kuu Kanda ya Bukoba imeahirisha kesi inayowakabili washtakiwa tisa wa kesi ya mauaji ya Asimwe Novart, mtoto aliyekuwa na Ualbino ambaye aliuawa na baadhi ya viungo vyake kukutwa vimenyofolewa wilayani Muleba mkoani Kagera mwezi Mei mwaka huu.

Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Bukoba, Emmanuel Ngigwana amechukua uamuzi wa kuahirisha kesi hiyo baada ya mshtakiwa namba moja Padri Elpidius Rwegoshora kutoonekana mahakamani ikidaiwa bado hajarejeshwa kutoka Taasisi ya Isanga iliyopo mkoani Dodoma alikopelekwa kwa ajili ya kufanyiwa vipimo vya afya ya akili.

Pia , Soma:
+ Watuhumiwa 9 wa mauaji ya Asimwe wadai hawajui kosa lao
+ Shahidi adai Padri Rwegoshora aliahidi kumpa V8 baba wa Mtoto Albino 'Asimwe'

Awali , wakili wa Serikali Erick Mabagala aliiomba mahakama kujua mustakabali wa mshtakiwa huyo ambaye Oktoba 25, 2024 kupitia kwa wakili wake Projestus Mulokozi aliiomba mahakama imruhusu aende katika Taasisi ya Isanga ili afanyiwe uchunguzi wa afya ya akili ,ombi ambalo mahakama iliridhia.

Jaji Ngigwana alikiri kupokelewa kwa ombi hilo na kwamba mahakama ilitoa siku 42 za ruhusa kwa mshtakiwa ili aende kufanyiwa vipimo lakini ameshindwa kurejea Bukoba kuendelea na kesi yake na kwamba Msajili wa Mahakama anafanya mawasiliano na Taasisi ya Isanga ili kujua hatma ya mshtakiwa huyo.

Baada ya mashauriano baina ya mawakili wa utetezi na wale wa Jamhuri, ndipo mahakama ilipoamuru kesi hiyo kuitwa tena Februari 17, 2025, huku washtakiwa wengine 8 wakirejeshwa rumande.

1733914572458.png

1733914590929.png
 
Mahakama Kuu Kanda ya Bukoba imeahirisha kesi inayowakabili washtakiwa tisa wa kesi ya mauaji ya Asimwe Novart, mtoto aliyekuwa na Ualbino ambaye aliuawa na baadhi ya viungo vyake kukutwa vimenyofolewa wilayani Muleba mkoani Kagera mwezi Mei mwaka huu.

Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Bukoba, Emmanuel Ngigwana amechukua uamuzi wa kuahirisha kesi hiyo baada ya mshtakiwa namba moja Padri Elpidius Rwegoshora kutoonekana mahakamani ikidaiwa bado hajarejeshwa kutoka Taasisi ya Isanga iliyopo mkoani Dodoma alikopelekwa kwa ajili ya kufanyiwa vipimo vya afya ya akili.

Awali , wakili wa Serikali Erick Mabagala aliiomba mahakama kujua mustakabali wa mshtakiwa huyo ambaye Oktoba 25, 2024 kupitia kwa wakili wake Projestus Mulokozi aliiomba mahakama imruhusu aende katika Taasisi ya Isanga ili afanyiwe uchunguzi wa afya ya akili ,ombi ambalo mahakama iliridhia.

Jaji Ngigwana alikiri kupokelewa kwa ombi hilo na kwamba mahakama ilitoa siku 42 za ruhusa kwa mshtakiwa ili aende kufanyiwa vipimo lakini ameshindwa kurejea Bukoba kuendelea na kesi yake na kwamba Msajili wa Mahakama anafanya mawasiliano na Taasisi ya Isanga ili kujua hatma ya mshtakiwa huyo.

Baada ya mashauriano baina ya mawakili wa utetezi na wale wa Jamhuri, ndipo mahakama ilipoamuru kesi hiyo kuitwa tena Februari 17, 2025, huku washtakiwa wengine 8 wakirejeshwa rumande.
Case closed
 
Back
Top Bottom