Bukoba: Maduka na biashara kwa ujumla zafungwa

Bukoba: Maduka na biashara kwa ujumla zafungwa

ichumu lya

JF-Expert Member
Joined
Aug 11, 2016
Posts
2,651
Reaction score
2,790
Katika hali isiyo ya kawaida Mkurugenzi ameamua kufunga maduka ya Bukoba Manispaa kutokana na mgogoro wa Leseni na service levy.

Hali hii imetokana na aliyekuwa afisa biashara Richard kugushi vitabu vya Reciept na kutoa Leseni hewa lakini amekuwa akilindwa licha ya ushahidi wote kuwekwa hadharani na wanachofanya kwa sasa ni kumuhamishia maeneo kama Ngara, Karagwe na maeneo mengine huku Mkurugenzi akidai hatambui leseni hizo mpaka kulipa tena miaka miwili mtawalia.

Mpaka sasa hali ni tete na hakuna kiongozi aliyejitokeza kuzungumzia kadhia hii huku wakiwaonga waandishi wa habari.

IMG_20221121_121928_504.jpg
IMG_20221121_122033_207.jpg
IMG_20221121_121909_517.jpg
IMG_20221121_121833_842.jpg
Screenshot_20221120-211328.jpg
IMG_20221119_130623_755.jpg
 
Tungoje yule mkuu wa kaya ya BK amtandike mkurugenz viboko kama alivyowafua wale wanafunzi kipindi kile.
Kwenye ndege alitudanganya, tusuburie na hapa pia. Au apatikane majaliwa mfungua kufuli.
 
Tungoje yule mkuu wa kaya ya BK amtandike mkurugenz viboko kama alivyowafua wale wanafunzi kipindi kile.
Kwenye ndege alitudanganya, tusuburie na hapa pia.
Au apatikane majaliwa mfungua kufuli
Kibaya zaidi wiki iliyoisha tu Rais kazuia TRA kufungia biashara saaa uyu mkurugenzi sijui anatumia akili gani.
 
Bukoba bwana, wanavyokuwa serious kukusanya mapato.

Maendeleo sasa hadi kuweka pavements stendi ya Bukoba wameshindwa. Sijui hela wanazipelekaga watu.

Ukiwa mkazi wa Bukoba na mfanyabiashara hata ule mwamko wa kulipa kodi unaisha kabisa kwa sababu matatizo sugu yanayoukumba mji huu huwa hayatatuliwi miaka nenda rudi.

Ukifika soko kuu Bukoba wata wanakamliwa kodi kweli kweli...lakin soko liko vile vile yaan mabanda toka nazaliwa hadi pele nitakapokufa nadhani.
 
Nimefuatilia kifungu cha sheria anachotumia nikagundua kilipitishwa na Ccm kwa mbwembwe leo kinawaumiza ata wao nashindwa kuelewa akili za watu wa Ccm wakiwa Bungeni.

Kodi hii ni matokeo ya Sheria ya fedha namba 9 ya 1982 kifungu cha 6 (1)(U).

Kodi hii hulipwa na makampuni, taasisi na biashara mbalimbali zilizosajiliwaVAT. Kutokana na mauzo ghafi kwa kiwango kisichozidi asilimia 0.3.

Kwa kawaida kodi hii hukusanywa mara nne kwa mwaka kila baada ya miezimitatu na utaratibu wa malipo ni kama ifuatavyo:-

· Mlipakodi Atatakiwa awasilishe hesabu ya mauzo yake katika Ofisi zaHalmashauri, ambapo atawakabidhi wataalamu wa kutoza kodi hiyo ambao baada yakuzidisha na hiyo asilimia 0.3 atalipa kiasi kinachopatikana.

Mfano mfanyabiashara ameuza kiasi cha Shs. Milioni moja kwa miezi mitatu,i.e. 1,000,000/= itazidishwa na asilimia 0.3 ambazo ni:- 1,000,000 x 0.3 kiasikinachopatikana yaani Shs. 3,000/= ndizo anazopaswa kulipa, na katika ulipaji,mlipa kodi anajaza fomu maalumu ambazo zinapatikana katika Ofisi za Halmashaurina kuambatanisha na mauzo yake na baada ya kufanya malipo anapewa risiti ambayoanapaswa kuiweka tika kumbukumbu zake kwa ajili ya ukaguzi n.k.

Aina ya Makosa yatakayosababisha kutozwa faini/adhabu:-

· Mtu yoyote anayetakiwa kulipa kodi akishindwa kuwasilisha hesabu zakekama inavyotakiwa kwa mujibu wa Sheria ndogo na inapobainika kuwa amefanyamakundi.

· Kodi ambayo haijalipwa kwa wakati kama ilivyoelezwa kwenye Sheriandogo itatozwa na riba ya faini ya asilimia kumi na tano (15%) kwa mwezina zitatakiwa kulipwa pamoja na kodi inayodaiwa.

· Mtu yoyote ambaye bila sababu za msingi atashindwa:-

(a) kuwasilisha nyaraka, maelezo au taarifa inayotakiwa kuwasilishwakwa Halmashauri katika muda uliowekwa.

(b) Kutunza kumbukumbu, kitabu au hesabu.

(c) Kuonyesha kumbukumbu yoyote au nyaraka kwa ajili ya uchunguzi.

Mtu yeyote bila sababu za msingi:-

(a) Akifanya hesabu za uongo kwa kupunguza au kutoa hesabu zisizokuwasahihi.

(b) Akitoa taarifa isiyokuwa sahihi kuhusu jambo lolote linalowezakuathiri jukumu lake au la mtu mwingine la kulipa kodi.

(c) Akiandaa au kutengenezewa vitabu vya uongo vya Mahesabu aukumbukumbu.

(d) Atamzuia au atajaribu kumzuia Afisa Muidhiniwa kutekeleza majukumuyake aliyopewa kwa mujibu wa Sheria ndogo atakuwa anatenda kosa.

Mtu yeyote atakayevunja masharti ya Sheria ndogo hizi atakuwa anatenda kosana atawajibika kulipa faini isiyozidi shilingi elfu hamsini (50,000/=) au kifungocha miezi isiyozidi (12) kumi na mbili jela au adhabu zote mbili kwa pamoja.

NB: Pamoja na adhabu atakayotozwa mkosaji kwenye kif.Na. 17 (1). Pia atawajibika kulipa gharama nyingine za Halmashauri.
 
Katika hali isiyo ya kawaida Mkurugenzi ameamua kufunga maduka ya Bukoba Manispaa kutokana na mgogoro wa Lessen na service levy. Hali hii imetokana na aliyekuwa afisa biashara Richard kugushi vitabu vya Reciept na kutoa Lessen hewa lakini amekuwa akilindwa licha ya ushahidi wote kuwekwa hadharani na wanachofanya kwa sasa ni kumuhamishia maeneo kama Ngara, Karagwe na maeneo mengine uku Mkurugenzi akidai hatambui lessen hizo mpaka kulipa tena miaka miwili mtawalia. Mpaka sasa hali ni tete na hakuna kiongozi aliyejitokeza kuzungumzia kadhia hii uku wakiwaonga waandishi wa habari.View attachment 2423101View attachment 2423102View attachment 2423103View attachment 2423104View attachment 2423105View attachment 2423106
kwenye wakiwaonga sjaelewa umemaanisha nini.
je kosa ni la nani kati ya wafanyabiashara na Richard?
 
Bukoba ndiyo sehemu pekee inayotumiwaga na serikali kutest sheria kandamizi ukikatiza Bukoba basi wanajua maeneo mengine ni mteremko.
 
Ukilipa Kodi unakuwa serious na Biashara...asikwambie mtu kulipa Kodi kunauma Sana....

Natamani nisilipe lkn roho inaniambia ipo siku Tin namba yako itakuwa na Madeni mengi na huku ukitamani kufanya Michongo ya maana ....hapo naamka na kwenda kulipa....


Kulipa Kodi kunauma Sana...
 
kwenye wakiwaonga sjaelewa umemaanisha nini.
je kosa ni la nani kati ya wafanyabiashara na Richard?
Mkuu mpaka apo hujaona kosa nilanani? Serikali inamlinda muhujumu uchumi inawakandamiza wananchi uyu Richard amekaa ndani baada ya GAG kubaini wizi uo 1998-2021 akaondolewa osifini lakini alipotoka ndani ameuza majumba yake na magari na mahakamani hakupelekwa kuna dalili zote za Rushwa kuwapoza viongozi ukizingatia alikua anasapoti sana Ccm.
 
Ukilipa Kodi unakuwa serious na Biashara...asikwambie mtu kulipa Kodi kunauma Sana....

Natamani nisilipe lkn roho inaniambia ipo siku Tin namba yako itakuwa na Madeni mengi na huku ukitamani kufanya Michongo ya maana ....hapo naamka na kwenda kulipa....


Kulipa Kodi kunauma Sana...
Acha mkuu ili ulinde account yako /TIN lazima ulipe ila likija swala la kuibiwa ulicho kimeibiwa inakuwa kasheshe
 
Kuibiwa Ni moja ya risk za Biashara,,,hasa Zama hizi tulizojaa wapenda shortcut
Acha mkuu ili ulinde account yako /TIN lazima ulipe ila likija swala la kuibiwa ulicho kimeibiwa inakuwa kasheshe
 
Back
Top Bottom