Mkalukungone mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 862
- 1,755
Jamani mambo yanatisha unyama unaofanywa na baadhi ya watu.
Sasa mtoto mchanga kabisa hii ni wazi ni imani za kishirikina tu zimefanyika na kutumika kwenye haya mauwaji!
===============
Mtoto mchanga, Antidius Avitus (miezi minne) amekutwa amefariki dunia na baadhi ya viungo vya mkono wake vikiwa vimenyofolewa huku bibi yake wa kambo akihusishwa.
Mauaji hayo yametokea Nkindo, Kijiji cha Itahwa, Kata ya Karabagaine, Manispaa ya Bukoba.
Akizungumza na Mwananchi leo Jumapili Novemba 11, 2024, mama wa mtoto huyo, Dorice Avitusi amesema tukio hilo lililotokea Jumamosi Novemba 9, 2024.
Amesema jana asubuhi alikuwa na mwanawe akiwa mzima na alimwandalia uji kabla ya kwenda naye kanisani kufanya usafi.
Anasema alirejea nyumbani mchana akiwa amembeba mgongoni akiwa amelala na akapitiliza kwenda kumlaza chumbani.
Soma Pia: Dodoma: Mtoto wa miaka minne akutwa amefariki baada ya kukatwa mkono na sehemu za siri
Akisimulia huku akibubujikwa machozi, Dorice amesema alienda dukani na aliporudi akaendelea kupika chakula cha mchana huku mtoto akiwa kalala.