Bukoba: Mwanamke auawa kwa kunyongwa na wanaodaiwa kuwa 'michepuko' yake

Bukoba: Mwanamke auawa kwa kunyongwa na wanaodaiwa kuwa 'michepuko' yake

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Jeshi la Polisi linawashikilia watu wawili kwa tuhuma za mauaji ya Editha Andason, mkazi wa Mtaa wa Kilimahewa, uliopo Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera, aliyeuawa kwa kunyongwa kwa mtandio shingoni.

Akizungumza na vyombo vya habari leo Desemba 28, 2024, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Brasius Chatanda amesema wamefanikiwa kuwakamata watu wawili waliokuwa wakitafutwa kwa tuhuma za mauaji ya mwanamke huyo.

Watuhumiwa hao wanaoshikiliwa Kituo cha Polisi Bukoba ni Mtalewa Answali pamoja na Kennedy Muganyizi, wote ni wakazi wa Mtaa wa Kashenye, kata Kashai na inadaiwa wote walikuwa na uhusiano wa kimapenzi na marehemu Editha.

Soma, Pia: Tabora: Mwanamke auawa, chanzo wivu wa mapenzi

Chatanda amesema watuhumiwa hao wanadaiwa kufanya tukio hilo Desemba 12, 2024 katika maeneo ya Mtaa wa Kilimahewa baada ya kugundua kuwa wote wapo kwenye uhusiano wa kimapenzi na mtu mmoja.

Taarifa ya Kamanda Chatanda imedai kuwa Editha alikuwa na mume ambaye ni dereva bodaboda, baadaye akaanzisha uhusiano wa kimapenzi na mwenzake waliyekuwa wakifanya kazi sehemu moja, ambaye ni Mtalemwa Answali.
 
Mshahara wa dhambi ni mauti!
Apumzike kwa amani.
 
Back
Top Bottom