Baadhi ya walimu wilaya ya Bukombe wameripotiwa kuzihama nyumba walizojengewa na Serikali na kwenda kupanga mjini Ushirombo kutokana na kuona mauzamauza ya sungura waliovaa tai na watu waliosimama katika nyumba hizo usiku. Hayo yamebainishwa katika kikao cha baraza la madiwani.
Chanzo: Clouds Media
Your browser is not able to display this video.
=====
Na inasemekana kuwa hata Mtanzania Mwenzetu Mmoja ( sasa amepumzika daima Milele ) japo Usoni alikuwa akionyesha ana Yesu Kristo, Roho Mtakatifu na Bikira Maria ila kwa haya ' Mauzauza ' na Yeye alikuwa ni Mdau Mkubwa kiasi cha Kuyaamini kuliko hata Sayansi yake ya Kikemikali pale COET ( UDSM )
Yule Dada mrembo na Mbunge wa Mlimba Itabidi aombe Mwongozo wa Spika juu ya hili, Ahoji uharali wa Mbunge yule aliependekeza mpaka yeye akatolewa Mjengoni, Isije nae ikawa alirukwa akili kama hawa wanaoona Sungura Kavaa tai [emoji23]
Uchawi upo, uamini au usiamini, haibadilishi chochote kile, uchawi upo na umekuwepo duniani kwa miaka mingi sana.
Jambo la muhimu ni namna gani unapambana na uchawi. Lakini kusema uchawi haupo ni kujidanganya.
Sisi Wakristo tunafahamu kuwa hata Biblia imetuambia kuhusu uchawi hivyo tunajua kuwa uchawi upo lakini tunaushinda kwa IMANI YA YESU KRISTO.