Nia ya challenge hii ni kubadili mawazo mgando ya kuwa bila mamilioni huwezi kuishi sio kweli.
Wakati unangoja hayo mamilion tafuta buku basi usionekane mzigo kwa wengine.
Jibu langu hilo hapo chini.
Nipe jibu lako na repost io picha uone mawazo ya vijana wenzio??
#Buku10challlenge
View attachment 1470443View attachment 1470445
Watu wa dsm ni rahisi sana buku 10 kufanyia biashara na baadae akikwambia mtaji unakataa.
Kuna biashara kama hiyo ya juisi (japo hii inategemea vifaa vinavyogharimu zaidi ya hiyo hela)
Kuna kuchoma mahindi, kuuza uji
Lakini halisia kabisa ambayo buku 10 ni mtaji mkubwa sana ni kukodi mkokoteni na kuuza maji (kuna jamaa namfahamu wakati huo miaka ya 2011 , alioa mke na akafanya harusi ya ukumbini (wa kishikaji), akanunua kiwanja na 2016 akasimamisha mjengo kwa biashara hiyo hiyo ya maji aliyokuwa anafanyia maeneo ya tabata)
Huyu jamaa alianza kwa kukodi mkokoteni wa kubeba madumu kumi na na madumu yake
Baada ya kuoa, alimfungulia mke genge yeye akaendelea kukomaa na maji. Hadi sasa jamaa anamiliki cary na boda boda mbili
Hapa tatizo ni moja tu kwa hiyo biashara, vijana wengi tuliojazana humu ni ngumu sana kusukuma mkokoteni na kuuza maji mtaani, humu wengi tulilogwa na ule ugonjwa unaopandikizwa darasani wa white collar jobs!
Nyingine (ambayo yoyote anaweza kufanya) ni kuuza matunda
Mwaka 2010 niliwahi kumkopesha ndugu yangu Tsh.30,000 ya boom akawa anafuata machungwa buguruni anauza mtaani (wale wanaomenya)
Ndani ya wiki mbili akanirudishia pesa yangu. Baada ya kama miezi mitatu biashara ilikuwa imeshakuwa kubwa na alikuwa na bidhaa tofauti tofauti. Baadae akamkabidhi dogo hiyo biashara yeye akaingia kwenye biashara ya mitumba. Hapa chanzo lilikuwa elfu 30 yangu niliyomkopesha tena ya boom.
Swali niulize yeye anaingiza shilling ngapi na Mimi naingiza shilling ngapi kwa siku!? Hapa utakuwa unanitaka ugomvi.
Kikubwa kwenye biashara ni uthubutu na ujasiri wa kufanya unachoona unakiweza.
Hata hivyo, yote hayo yanabebwa na eneo ulilopo. Sisi tulio mikoani au kwenye miji midogo kuna biashara haziwezekaniki na ni ngumu kukupa faida. Kwa mtazamo wangu walioko DSM wana advantage kubwa ya kufanya chochote japo haitakiwi iwe kigezo cha sisi tusio dsm kushindwa kufanya chochote. Ni vizuri kutafuta kinachowezekana ndani ya mazingira uliyopo