Buku 10 challenge: Unaweza kufanya biashara gani kwa pesa hiyo na ukaishi?

Mahindi ya kuchoma/
Buku saba jelo nanunua mahindi ya kuchoma kwa 150tsh× pc 50 =7,500/=tsh
Inabaki 2,500/=tsh pesa ya mkaa wa kuchomea mahindi pamoja na malimao na chumvi.

Hindi moja ni 500/=tsh mpaka 700/=tsh,ila ukifanya maxmum ya 500/=tsh kila pc 50 jumla ya mauzo yatakuwa 500tsh ×50pc =25,000/tsh.ukitoa elfu kumi na tano ya mtaji na chakula 25,000-15,000=10,000/tsh.faida
 
Kikubwa ni usiangalie hiyo fedha kwamba ni kubwa au ndogo. Ukitaka kuwa tajiri angalia umehudumia watu kiasi gani kutatua matatizo yao wakakulipa. Hivyo badilishana thamani na watu million moja kila mmoja akupe sh 100. Utakuwa na mil100.
 
Kikubwa ni usiangalie hiyo fedha kwamba ni kubwa au ndogo. Ukitaka kuwa tajiri angalia umehudumia watu kiasi gani kutatua matatizo yao wakakulipa. Hivyo badilishana thamani na watu million moja kila mmoja akupe sh 100. Utakuwa na mil100.
Exactly, ndio maana kina Mengi wametarget Tshs. 300 kwenye naji na soda ila kwa wingi wa carton zinazonunuliwa kwa week/Mwezi/Mwaka zimeweza kuwafanya Multi-Millionaires kwa muda mchache tu!

Extend your distribution spots ili kufikia watu wengi then Boom!
 
Kuuza fegi
Utapata fedha lakini je ni tatizo umetatua au umezidisha matatizo? Kwanza zinachafua mazingira, na zinaleta magonjwa ya kansa, vifua na madhara mengine mengi. Hapa hujatatua tatizo
 
Watu wa dsm ni rahisi sana buku 10 kufanyia biashara na baadae akikwambia mtaji unakataa.

Kuna biashara kama hiyo ya juisi (japo hii inategemea vifaa vinavyogharimu zaidi ya hiyo hela)

Kuna kuchoma mahindi, kuuza uji

Lakini halisia kabisa ambayo buku 10 ni mtaji mkubwa sana ni kukodi mkokoteni na kuuza maji (kuna jamaa namfahamu wakati huo miaka ya 2011 , alioa mke na akafanya harusi ya ukumbini (wa kishikaji), akanunua kiwanja na 2016 akasimamisha mjengo kwa biashara hiyo hiyo ya maji aliyokuwa anafanyia maeneo ya tabata)
Huyu jamaa alianza kwa kukodi mkokoteni wa kubeba madumu kumi na na madumu yake

Baada ya kuoa, alimfungulia mke genge yeye akaendelea kukomaa na maji. Hadi sasa jamaa anamiliki cary na boda boda mbili

Hapa tatizo ni moja tu kwa hiyo biashara, vijana wengi tuliojazana humu ni ngumu sana kusukuma mkokoteni na kuuza maji mtaani, humu wengi tulilogwa na ule ugonjwa unaopandikizwa darasani wa white collar jobs!

Nyingine (ambayo yoyote anaweza kufanya) ni kuuza matunda

Mwaka 2010 niliwahi kumkopesha ndugu yangu Tsh.30,000 ya boom akawa anafuata machungwa buguruni anauza mtaani (wale wanaomenya)

Ndani ya wiki mbili akanirudishia pesa yangu. Baada ya kama miezi mitatu biashara ilikuwa imeshakuwa kubwa na alikuwa na bidhaa tofauti tofauti. Baadae akamkabidhi dogo hiyo biashara yeye akaingia kwenye biashara ya mitumba. Hapa chanzo lilikuwa elfu 30 yangu niliyomkopesha tena ya boom.

Swali niulize yeye anaingiza shilling ngapi na Mimi naingiza shilling ngapi kwa siku!? Hapa utakuwa unanitaka ugomvi.

Kikubwa kwenye biashara ni uthubutu na ujasiri wa kufanya unachoona unakiweza.

Hata hivyo, yote hayo yanabebwa na eneo ulilopo. Sisi tulio mikoani au kwenye miji midogo kuna biashara haziwezekaniki na ni ngumu kukupa faida. Kwa mtazamo wangu walioko DSM wana advantage kubwa ya kufanya chochote japo haitakiwi iwe kigezo cha sisi tusio dsm kushindwa kufanya chochote. Ni vizuri kutafuta kinachowezekana ndani ya mazingira uliyopo
 
Yap idea nzuri sana..tuendelee kuwafungua akili wenzetu wanaongojea wapte kodi za frem
 
Buku 10 uza bangi.

Puli moja elfu 3, nunua puli tatu elfu 9 elfu moja iliyobaki nunua rizla.

Puli moja linatoa bangi hamsini, bangi moja uza mia 5, 500×50=25000

Kwa mapuli matatu 25000×3=75000

Ukitoa buku ten yako ya mtaji unabakiwa na faida ya elfu 60
 
Maeneo ya kitunda ipo wapi?
Kitunda sijawahi kuishi so sijui. Sehemu ya mbali kufuata gym ilikua Gongo la Mboto, gharama ilikua 50K kwa mwezi.

Najua Kawe, Makumbusho, Mwananyamala, Kigamboni, Ujiji, Tandale
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…