Bulawayo, Zimbabwe 1993

Jambo manolo sahau au msilolijua ukijaribu kuenda kinyume na maslahi ya wazungu wanakutengenezea mazingira ushindwe na uonekane hauwezi kitu na ulikosea kujitoa kwenye makucha yao ya kinyonyaji au unyanyasaji.

Utapigwa vijwazo usiweze kujitegemea au kuendelea na kuendeleza waliyokuachia.

Kiufupi wana kutengenezea mazingira ya kushindwa.
 
Mkuu kwangu huu ni upumbavu wa sisi black people kuwa mpaka leo tunalaumu white peoples kwa fails zetu,nchi nyingi zinazoongozwa na watu weusi zimekua failed state, dictator Mugabe aliichukua Zimbabwe ikiwa ni super, few years down the line nchi imekua ni mess, why Mauritius, ushelisheli,Botswana, Namibia na sasa Ghana they're getting right ✅, the rest of Africa ni shida tupu, let's talk as it's, sugar coating issues ndio imetuleta hapa,uongo na unafiki na kusifia sifia upuuzi.
 
Nilipita Bulawayo ilikuwa 1998 nikielekea Johannesburg, wakati tunasubiri bus tulikuwa tunaongelea vuguvugu la kisiasa pamoja na mgogoro wa ardhi unaoendelea pale Zimbabwe, nakumbuka Kondakta alinambia " brother this country is going to be like Somalia" by that time Zimbabwe ilikuwa nchi nzuri, nakumbuka tulikuwa hatupendi kupoteza muda Zambia, haraka tunachukua usafiri wa kutupeleka Harare.

Sent from my TECNO KD7 using JamiiForums mobile app
 
Umenikumbusha mbali sana. Nilienda Zimbabwe miaka 10 baada ya Uhuru wao. Nikaenda tena 2000, miaka 20 baada ya uhuru wao. Nilitumwa kufanya viutafiti vidogo vidogo vya kibiashara.

Zimbabwe ya miaka 10 baada ya uhuru ilikuwa nzuri sana, miaka 10 mingine tena, ilibaki vilevile bali kulikuwa na athari za kuchoka choka baadhi ya huduma.
 
bi Faiza u mzima weye
 
Nimeishia hapo!!!!!! Nilijua lazima kila andiko uweke SYKES
 
Nimeishia hapo!!!!!! Nilijua lazima kila andiko uweke SYKES
Naru...
Vipi utaacha kumtaja Kleist Sykes ikiwa historia ni kuhusu uasisi wa African Association mwaka wa 1929.

Vipi utaacha kumtaja Abdul Sykes kama ni kuingia uongozi wa vijana TAA 1950 President Dr. Vedasto Kyaruzi na Secretary Abdulwahid Sykes.

Vipi utaacha kumtaja Ally Sykes ikiwa yeye ndiye alikuwa akiandikiana barua na Kenneth David Kaunda mwaka wa 1953.

Vipi utaacha kumtaja Abdulwahid Sykes ilhali yeye ndiye aliyempokea Julius Nyerere Dar es Salaam 1952.

Vipi utaacha kuwataja Abdul na Ally Sykes ikiwa hawa ndugu wawili ni kati ya waasisi 17 wa TANU na baba yao ndiyo mwasisi wa TAA.

Ukisema uwafute hawa ndugu wawili na baba yao katika historia ya uhuru utabakia na historia gani ya kweli?

Unadhani hakuna ulazima wa kuwataja akina Sykes?

Hebu angalia video hii:


View: https://youtu.be/CGMTMFKMzB8?si=-IG19tOYNMqjhyMK
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…