DIZZO MTAWALA
JF-Expert Member
- Aug 22, 2015
- 240
- 767
Kwa nini mjadala wa Katiba ni muhimu?Sababu ni kuwa.
1.Hii ya 1977 iliandikwa ili kuuimarisha mfumo wa siasa za Chama kimoja na ililenga kukifanya chama cha Siasa kuwa juu ya hata Mihimili ya dola.
2.Iliandikwa ili kuhakikisha tunajenga taifa ambalo njia kuu za Uchumi zinakuwa chini ya miliki ya dola kwa kutumia mifumo ya uchumi wa ujamaa.
3.Iliandikwa bila kuwashirikisha wananchi, mwaka 1977 kulikuwa na majukumu mawili kuandika Katiba ya CCM na ile ya Nchi.
N.B
Zilikuwepo sababu za msingi kufanya hivyo kwa wakati huo.
1.miaka 5 nyuma taifa lilikuwa limepita kwenye misukosuko mingi ya kiusalama likiwepo suala la kifo cha Rais wa Zanzibar mwaka 1972.
2.Dunia ilikuwa kwenye vita baridi
3.Oparesheni vijiji vya ujamaa ilikuwa imeanza kufifisha umaarufunwa serikali na chama.