Bunda High School inahujumu shule jirani kwa kurubuni na kuchukua wanafunzi wao mahiri

Bunda High School inahujumu shule jirani kwa kurubuni na kuchukua wanafunzi wao mahiri

Mjukuu wa kigogo

JF-Expert Member
Joined
Sep 19, 2023
Posts
445
Reaction score
1,094
Bunda high school zamani ikijulikana kama Bunda day ilianzishwa kama shule ya tarafa mwaka 1990. Tunaweza kusema ni kati ya shule kongwe wilayani Bunda.

Kwa sasa ina vidato vyote kuanzia kidato cha kwanza mpaka cha sita. Ni shule yenye walimu wa kutosha, miundombinu ya kutosha na kama haitoshi ni kati ya shule zinazotoa motisha nzuri kwa wafanyakazi wake huku ikichagizwa na uwepo wa uongozi Bora.

Tatizo lipo wapi Sasa?
Tuendelee.....,

Ushindani wa kitaaluma katika shule nyingi zilizo jirani ulipelekea shule hii kuanza kuzifanyia michezo michafu shule jirani kwa kurubuni wanafunzi wenye uwezo kitaaluma kutoka shule hizo ili kuhamia shule husika. Ipo hivi mara tu matokeo ya mitihani ya kidato cha tatu yanapotoka mwisho wa mwaka baadhi ya walimu huendesha operation ya kuwatafuta wazazi wa watoto cream waliopata ufaulu mzuri ( division one) na kuwapa ahadi kedekede endapo watahamishia watoto wao katika shule ya Bunda high school.

Hili huenda sambamba na kuonyesha udhaifu wa shule jirani. Hili limekuwa likifanikiwa kwa zaidi ya 98%.

Baada ya hapo nini hutokea?
Zoezi hili linaweza kukusanya idadi ya watoto 20 au zaidi na shule inakuwa na mtaji wa ziada wa uhakika wa kupata division one 20+ katika mitihani wa Taifa kidato cha nne za wahamiaji tu ambapo ukijumlisha na walioanzia hapo shuleni shule inakuwa na division one 40+.

Hii ni mission ambayo ilisukwa kiustadi ndani ya miaka 10 iliyopita na muasisi wake akiwa mwalimu moja wa somo la Biology kwa jina la "G"

Kwanini niseme siyo fair?
Shule jirani kama Sazira, Nyiendo, Dr. Nchimbi na Rubana zimejikuta zikipoteza wanafunzi mahiri ambao wanakuwa tayari washarubuniwa kuhamia hapo na matokeo yake walimu husika katika shule hizo huonekana hawatimizi majukumu Yao ipasavyo!

Wito wangu andaa vizuri wanafunzi wako na jirani naye aandae vizuri wa kwake muwe na ushindani ulio fair,otherwise mnakuwa mnahujumu walimu wenzenu.
Asanteni

Nakazia

Zoezi hili lipo katika maeneo mawili:
Wale waliopata division one kwenye mtihani wa kidato cha pili (Ftna) ambapo wao huhamia kidato cha tatu bunda high school.

Wale waliopata division one mtihani wa mwisho wa mwaka(annual examinations) wakiwa kidato cha tatu ambao huhamia na kuanza maisha kidato cha nne Bunda high school
 
Shida hiko wapi? Tunajenga nyumba moja tusigombanie fito! Muache awachukue uenda wangekaa kwao wangefeli!
 
Back
Top Bottom