Uchaguzi 2020 Bunda Mjini kumekucha viongozi wa CCM Wilaya waanza kushikana uchawi kwa sababu ya rushwa za Mwanza huduma

Uchaguzi 2020 Bunda Mjini kumekucha viongozi wa CCM Wilaya waanza kushikana uchawi kwa sababu ya rushwa za Mwanza huduma

chuki

JF-Expert Member
Joined
Mar 10, 2011
Posts
2,715
Reaction score
534
"Mmoja amlima barua mwenzake ili makao makuu waingilie kati" barua imeambatanishwa.

Hali inazidi kuwa tete Wilaya ya Bunda baada ya Viongozi wa CCM wilaya kushutumiana kula rushwa za Mtia Nia Zury Nanji maarufu kama Mwanza Huduma.

Viongozi hao wamefikia hatua mbaya ya kushutumiana na kuomba ofisi za CCM Makao makuu kuingilia kati ili kuinusuru ofisi hiyo maana pesa za Mhindi huyo ziwatia upofu na kukuta kila mmoja anatamani afanye kazi ya mwenzake ili kumfurahisha Mtoa pesa.

Kabla uzi huu haujapanda hapa tayari Mwenyekiti wa CCM Wilaya na Mwenezi wa CCM Wilaya wamewachukua kundi la Wanawake na kuwapeleka Mji mdogo wa Magu ili kufanya kampeni za kificho maana kila wanalofanya Bunda Mjini limekuwa likitoka haraka, Katika jukumu hilo ambalo limeongozwa na Mwanamke aitwae Theopista Machupa liliwakusanya wanawake wa UWT ili wakaonane na Mhindi huyo hapo Magu, chini ya usimamizi wa Mkiti na Mwenezi wa Wilaya.

Mtoa habari anasema kila Mwanamke alipewa Kitenge kimoja na Elfu Hamsini ili kumsaidia bwana Zury Nanji ambaye aliongea nao siku hiyo hapo Magu.

Katika Hali ya sintofahamu kundi hilo likiwa katika Hotel moja ya kificho Askari na Mgambo wa Operation ya kuzuia Mikusanyiko ya kuzuia Ugonjwa wa Corona waliwakurupua jambo ambalo lilimfanya Mkiti wa CCM Wilaya ya Bunda akurupuke kukimbia almanusura avunjike mguu akidhani kuwa ni Takukuru.

Zury Nanji amenunua ofisi nzima ya Chama na kuhonga kila mtu kitendo kilichomchefua Mkiti wa Vijana Wilaya na kuamua kuandika Barua Makao makuu ya CCM ili waingilie kati sakata la Milungula ndani ya chama.

IMG-20200329-WA0003.jpg
IMG-20200329-WA0004.jpg
Kabla ya uchaguzi wa kura za maoni tutashuhudia kila rangi, huku makundi ya wagombea yakishtumiana kutoboreana siri.
 
Kama mwenyekiti wa UVCCM wilaya ni mbovu wa kiswahili namna hii hata sishangai. Kama kuandika tu kiswahili hawezi, je ataweza kuongoza vijana kweli?
 
"Mmoja amlima barua mwenzake ili makao makuu waingilie kati" barua imeambatanishwa.

Zury Nanji amenunua ofisi nzima ya Chama na kuhonga kila mtu kitendo kilichomchefua Mkiti wa Vijana Wilaya na kuamua kuandika Barua.

View attachment 1403603View attachment 1403604Kabla ya uchaguzi wa kura za maoni tutashuhudia kila rangi, huku makundi ya wagombea yakishtumiana kutoboreana siri.

Suala la rushwa katika hatua hizi za uchaguzi hasa ndani ya CCM (kwakua mimi ni mwanachama nina uzoefu navyo) lilishazoeleka na kuna hatua linaonekana suala la kawaida kabisa, japo nashindwa kuelewa dhana ya “CCM Mpya” kama ina mkakati wa kulimaliza hili.
Lakini kwa upande mwingine nashindwa kutokukuchukulia pia kama sehemu ya propaganda kutokana na hiyo barua uliyoweka humu, haijasainiwa maana yake umeipata kutoka kwenye source kabla haijafika kwa mtu mwingine!! Lakini haina header ya chama pia. Isije kua na wewe unatumiwa na mtia nia mwingine kutaka uungwaji mkono.


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Huyo jamaa Nanji anatoa rushwa wazi namna hiyo ina maana vyombo vya usalama ikiwemo Takukuru hawajamuona?

Halafu wamezoea kuwakamata watoa rushwa ya laki moja na kuwatangaza waonekane kila mahali.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Niliwashauri CCM, waache watu wapewe fedha
Pascal pale Bunda napafahamu vizuri sana na siasa zao majitaka. Kila aliyepo CCM pale Bunda yupo kimaslahi so ukiona hivi ujue kuna mmoja kanyimwa au katengwa kwenye mgao.
Huyu mwenyekiti wa UVCCM walimchagua kwakufuata mkumbo maana hata form four hakumaliza. Zachinichini zinasema aliishia form two. Sasa huwa anajimwambafy sana na kujiona ndiye mwenye kura nyingi za vijana na kupenda kutukana watu wazima. Ndicho kilichomkuta sasa ameamua bora awe mmbea au amwage unga wote walale njaa kama kipindi cha Wasira na Esta Bulaya waliaanza hivihivi jimbo likapotea kwa wao kwa wao kufitiniana nadani ya jumuiya zao. Yeye anamuunga mkono jamaa anaitwa Pius sasa nguvu ya fedha inaonekana kumsukuma nje taratiiiiiibu.
 
Hizo ni hofu na nbinu mfu za mbunge wa sasa hapo bunda mjini!
Kama huyo mhindi chadema wamemuogopa waambie njama za kutaka kumchafua ili akatwe ! Zimebuma.
Atakuja huyohuyo mhindi mwambieni ndg yenu bulaya afungashe virago! Abakie kuhudhuria mahakamani .

Chadema tunaenda kuizika rasmi mkoa wa mara.
 
Mwanza huduma?
Ndio nani na anahudumia nini?
Anawahudumia akina nani?
Mwambie akahudumie tigo uko sisi uku Tupo bize na voda
 
Hizo ni hofu na nbinu mfu za mbunge wa sasa hapo bunda mjini!
Kama huyo mhindi chadema wamemuogopa waambie njama za kutaka kumchafua ili akatwe ! Zimebuma.
Atakuja huyohuyo mhindi mwambieni ndg yenu bulaya afungashe virago! Abakie kuhudhuria mahakamani .

Chadema tunaenda kuizika rasmi mkoa wa mara.
Mbona hii barua haina sahihi ya mwandishi?.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom