Bundi atua Mtaa wa Msimbazi hata Ligi kuu haijaanza, Kulikoni?

tramadol

JF-Expert Member
Joined
Oct 10, 2015
Posts
5,383
Reaction score
4,323
Naona Bundi ameshatua Msimbazi hata mzunguko wa kwanza haujaanza.

Simba mjipange kwa kuchukua Kombe na si kuanza kugombea kumiliki Timu.

Na hapo ndipo Yanga anapochukua nafasi na kuchukua Kombe tena msimu huu.

Naona maneno ya kibaguzi si mazuri Katika mikutano yetu.....Simba asili na Simba wahindi. Haya ni maneno ya kuyapiga vita kila iitwapo leo.

Sisi wote ni watanzania na tunaipenda nchi yetu na Mpira wetu.

Mungu ibariki Tanzania.
 
Hawa simbasaba ndio walivyo. Kila msimu hawakosi migogoro. kama sio kuhusu nidhamu ya wachezaji basi ni usajili wa wachezaji, ama la utakuta umiliki wa timu ndio chanzo, mara wanagombania hela ya usajili. Hawa watani wazembe waache kujitafutia sababu, wakomae watusaidie kubeba ndoo mwishowe tumechoka kubeba, azam wao msimu huu naoma hawana mpango wa ndoo.
 
Moto utawaka zaidi kama watafungwa na Yanga kwenye ngao ya hisani. Tuwaombee waje kushinda hiyo GAME.

Sent using Jamii Forums mobile app
Wanayanga mnaandika sana kuhusu Simba sc.
Yaani kila mahali mnaandika kuikosoa Simba sc.
Ivi mnamatatizo gani ?

Wakati wa Manji mlishatufunga nje ndani, yaani mechi zote mbili za ligi, mlipowatumia akina Kessy na Kiiza, Simba ilitulia tu.

Sasa hivi kila ukisoma site za mitandaoni utaona Yanga wanaandika kuikejeri Simba sc, mara Saba bila, mara Ubaguzi kwa wahindi na waarabu, mara Niyonzima.

Yaani ni kelele kila kukicha.
Kila mda mnaanzisha (thread) mada za kuikejeri Simba. Ivi Manji alikuwa mmakonde ?

Hamjifunzi kwa wenzenu Simba sc jinsi wanavyowapotezea tu na wala hawawaandikii mada nyingi za kuwakejeri.

Inaonekana wengi we mko vijiweni tu hamna cha kufanya zaidi ya kusogoa.

Au mnaihofia sana Simba sc na mnaiota kila wakati.

Mnaanza kuchosha mitandaoni hata kama ni utani nyie mmezidi sana.

Angalieni humu ktk Jamii forum, hakuna mada iliyoanzishwa inayoikejeri Yanga fc, kama ikiwepo basi moja au mbili.
Sasa mhesabu mada za Wanayanga kuidhihaki Simba sc, zinazodi kumi, na kila siku inatoka mpya.

I think there is something wrong in your fore-head.

Hefu fuatilieni timu yenu.
Mjipime na mjiongeze sasa.
 
Kamuangalie MZUNGU wenu Haji Manara instagram... Akilala Akiamka Yanga... Akinya akitawaza Yanga.. Yanga Muda wote Simba keshawasahau
 
Kamuangalie MZUNGU wenu Haji Manara instagram... Akilala Akiamka Yanga... Akinya akitawaza Yanga.. Yanga Muda wote Simba keshawasahau
Basi mjibuni hukohuko instagram. sasa huku forum atayaonaje majibu yenu ?

Jukwa la michezo la Jamiiforum sio mahali pa kusogoa habari za udaku.

Labda kule chichat.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…