Mbunge Salome Makamba ametaka serikali kuwalinda wateja wa simu za mkononi ambao wanabanwa na mikataba isiyo ya usawa, kuwalazimisha kutumia salio za vifurishi huku walaji hao wakiwa hawana mtetezi wa kuuliza makampuni ya simu dhima na sababu ya kulazimisha walaji kutumia vifurushi vilivyosalia .
Mbunge huyo amesema suala la kulazimisha wateja kumalizia salio halipo ktk nchi zingine zilizoendelea na kutaka TCRA / Ombudsman yaani ofisi ya kushugulikia malalamiko ya wateja wa simu za mkononi Tanzania kuwanusuru na adha hiyo ya kuburuzwa kwa kisingizio mkataba unawabana walioingia wakati wateja hawana nguvu kupingana na makampuni hayo makubwa ya simu.