Yoyo Zhou
Senior Member
- Jun 16, 2020
- 126
- 215
Trump, ambaye alijruhiwa kwa risasi, ni mgombea urais ambaye anaunga mkono kwa nia thabiti haki ya watu wa kawaida kuwa na bunduki. Aliahidi kuwa atalinda haki hiyo kama ataweza kuchaguliwa tena kuwa rais wa Marekani.
Ikiwa nchi yenye idadi kubwa zaidi ya watu wenye bunduki duniani, Wamarekani wa kawaida wana bunduki milioni 390, sawa na kila Wamarekani 100 wana bunduki 120.5, ambazo zimekuwa moja ya changamoto sugu zaidi ya kijamii nchini Marekani. Takwimu zinaonesha kuwa, hadi Julai 10 mwaka huu, watu 8,934 wamefariki kutokana na ghasia za ufyatuaji risasi nchini humo, na wengine 17,060 kujeruhiwa. Takwimu pia zinaonesha kuwa kati ya mwaka 2018 na 2023, wastani wa matukio makubwa ya ufyatuaji risasi yaliyosababisha vifo vya watu zaidi ya 4 nchini Marekani kwa mwaka ulikuwa 603, na kuleta hasara ya dola bilioni 557 za Kimarekani, ambayo ni kama asilimia 2.6 ya Pato la Taifa la nchi hiyo.
Wakati huo huo, Marekani pia inasafirisha maafa haya kwa nchi nyingine kupitia kuziuzia bunduki, na kusababisha tishio kubwa kwa usalama wa kijamii duniani.
Shirika la Habari la Marekani Bloomberg lilitoa ripoti ya uchunguzi, ikisema asilimia 37 ya bunduki zilizopatikana na kufuatiliwa katika matukio ya uhalifu katika nchi zisizo za bara la Amerika Kaskazini, zilisafirishwa kihalali kutoka Marekani, pamoja na bunduki zilizouzwa kwa njia haramu, kiwango hicho kinatisha zaidi.
Mwezi Oktoba mwaka 2022 mauaji ya kikatili yalitokea katika shule ya chekechea kaskazini mashariki mwa Thailand. Muuaji huyu aliwaua watu 36, wakiwemo watoto zaidi ya 20 wenye umri wa miaka kati ya 2 na 5. Bastola iliyotumiwa na muuaji huyo iliuzwa nchini Thailand na Kampuni ya Sig Sauer, ambayo ni kampuni kubwa zaidi ya kuuza bunduki nje ya Marekani. Mauzo ya bunduki za Marekani kwa nchi za nje yameongezeka maradufu katika kipindi cha miaka sita iliyopita, na Thailand ni moja ya nchi zilizoagiza zaidi bunduki hizo za Marekani. Takwimu zinaonyesha kuwa katika miaka hiyo sita, idadi ya matukio ya uhalifu yanayohusiana na bunduki nchini Thailand imeongezeka kwa asilimia 43.
Nchi jirani na Marekani zimeteseka zaidi kutokana na mauzo ya nje ya bunduki za Marekani. Kwa mfano, nchini Mexico, mwaka 2020, kati ya mauaji 24,600 yanayohusiana na bunduki, asilimia 70 na 90 ya bunduki hizo zilitoka nchini Marekani. Serikali ya Mexico ilikadiria kuwa hasara za kiuchumi kutokana na bunduki hizo zimekuwa dola bilioni 10 za Kimarekani. Wakati huohuo, idadi ya bunduki zinazoagizwa na Guatemala kutoka Marekani iliongezeka kutoka wastani wa takriban 3,600 kwa mwaka katika miaka ya 2010 hadi 20,000 mwaka 2022. Mauaji nchini humo ambayo yalikuwa yamepungua kwa miaka 11 mfululizo, yanaongezeka kila mwaka, na zaidi ya asilimia 80 ya mauaji hayo yanahusiana na bunduki.