Bunge, Katiba, Madaraka

Bunge, Katiba, Madaraka

Francis fares Maro

JF-Expert Member
Joined
Jun 20, 2021
Posts
1,227
Reaction score
1,339
Wasalaam

Bunge
Ili uwe mbunge lazima uwe mwanachama wa chama cha siasa,chama kina kupa dhamana,kama sivyo basi itokee utashi wa Raisi akuteue!!.. Mfumo wa Bunge letu na wabunge wenyewe ni tishio kama siyo kichekesho!!..hakuna sheria wanazotunga kwaajili ya serikali na wananchi na siyo kiwakilishi cha wananchi!!.. Mtu anagombea ili akatatue shida na matatizo yake binafsi siyo wananchi waliyo mchagua ndio maana unaona wabunge wa kuteuliwa wananguvu zaidi ya wale waliyogombea huko majimboni!!..

Bunge letu hakuna kuwajibishana endapo serikali au mmoja wapo kafanya ndivyo sivyo!!..Bunge la wasanii na bendera fwata upepo!!..Bunge linategemea Raisi kaamkaje na anataka nini hakika tumepatikana! Bora hata wakati mwengine spika anajitahidi kuficha aibu hii lakini hapa tumepigwa!!!..

Katiba
Katiba ndio uti wa Mgongo lakini ajabu ya katiba yetu (kila kiongozi anafwata matakwa yake siyo katiba inataka nini)..Bunge linaendeshwa na watu wachache Kwa maslahi Yao na familia zao!!..Raisi nae anafanya atakavyo akiona kuna sehemu kuna shida yeye anakanyaga tu who cares!!!..

Vyama vya Siasa
Msingi wa kuanzisha au kukubali mfumo wa vyama vingi vya Siasa ni kuonekana na wafadhili na kupata misaada ili tuweze kuishi siyo kupata viongozi Bora wanaoweza kutuletea maendeleo ya kweli.. Unaweza kujiuliza kwanini hivi, jaribu kuangalia kila mfumo wa vyama vyetu wa siasa na jinsi vilivyoanzishwa ni dhahili shahiri bado kuna tatizo kubwa!!..

COVID-19
Hebu waangaalie hawa kina mama na Dada zetu jinsi walivyocheza kete zao!!!..Bunge linajua kabisa hawa siyo wabunge na hawakustahili kuwepo ndani ya Bunge lakini Nani anahoji (who cares)..Angalia Bajeti yetu.

Angalia mambo yanavyokwenda sasa hivi kweli hawa hata kama walipita mlango wa Nyuma mbona wamekua kama wamefungwa midomo kabisa!!..wanajua mambo siyo shwari na wakitoa ushauri wowote wanakwenda na maji (ukila na kipofu usimshike mkono)

Katiba Mpya
Kila chama cha Siasa kinafikiria au kutaka kuchukua nchi (kutawala) ukiangalia madai ya katiba mpya utagundua kuna watu wanahitaji chakula Mezani lakini Nani wa kuwapelekea chakula hicho?!!...Haya makongamano ya katiba yangefanywa na taasisi za kiraia zisizokua za vyama vya Siasa nadhani tungekua tunaongea lugha moja sasa!!!..

Madaraka
Kwa mifumo ya nchi yetu nadhani kila mtu aombe Mungu apate Madaraka sasa maana Madaraka kwetu ndio kila kitu ukiwa na Madaraka (Mkuu wa mkoa,mkuu wa wilaya na wakurugenzi,wabunge na mawaziri,wakuu wa Taasisi za serikali etc) nchi hii ni tamu sana nadhani hakuna nchi nzuri na tamu kama hii!!...Yani wananchi masikini ndio wanalipa Kodi kwaajili ya mishahara na usafiri wa vibopa!!...
 
Katiba mpya

FB_IMG_1617624645655.jpg
 
Huwezi kuwa mbunge mpaka uwe mwana chama wa chama cha siasa na chama ndicho hukudhamini,baada ya hapo unaenda kuchaguliwa na wana nchi ili ukawasemeee bungeni dhidi ya muhimili wa serikali nakutunga sheria.Hapo sasa mwenyekiti wa chama chako aliye kudhamini ndiye mwenye serikali "rais"unapo mpelekesha huyu jamaa na serikali yake ukiwa bungeni ghafla Ana vaa kofia ya uenyekiti anakufukuza chama na ubunge wako unajoma.
TUSIWALAUMU SANA WABUNGE KATIBA MPYA NDIYO SOLUTION
 
Back
Top Bottom