Bunge kuwa na Wabunge kinyume na matakwa ya Katiba. Je, ni Bunge halali Kisheria?

Bunge kuwa na Wabunge kinyume na matakwa ya Katiba. Je, ni Bunge halali Kisheria?

Lord OSAGYEFO

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2021
Posts
3,085
Reaction score
4,890
Naomba wanasheria wetu Waliobobea kwenye Masuala ya Katiba watuelimishe kisheria. Je, Uwepo wa Wabunge kinyume na katiba ya nchi na Kushiriki vikao na Kuchangia hoja Mbalimbali na Kupitisha Misuada na Sheria mbalimbali huku Wakiwa Hawana SIFA za kuwa Wabunge Kutokana na kufukuzwa Uanachama Wao ndani ya chama chao Je bunge hilo ni halali kwa mujibu wa Sheria?
 
Kwani wale wafanyakazi waliofukuzwa kwa vyeti feki wako wapi Sasa??

Ukipata jibu ndio utajua na hao wabunge
walipaswa kuwa wapi
 
ULIZA PAPO KWA PAPO yupo bungeni humohumo.
Anapigiwa,
Anawapigia,
Majibu mwaaaa
Nilimsikia Mambosawa kamwambia Maelekezo mkuu''
 
Hapa ndiyo kukosekana kwa dhana ya Utawala Bora. Hakuna kuheshimu Katiba ya Nchi.
 
Linakuwa halina tofauti na mkutano wa hadhara wa kijiji.

Ni kwa vile taasisi za kijamii na kitaaluma kama TLS zimekufa na zinadhindwa kuhoji kwa kina jambo hilo.

Bunge hili linakosa uhalali wa kutu ga sheria. Inakuwaje jengo ambalo hata Rais anaingia kwa kibali wengine wanachaguliwa kuingia na spika kama wanaenda kujisaidia?
 
Tatizo liko kwenye katiba yetu mbovu. Kuwepo kwa uvunjwaji wa katiba wa wazi tena ktk bunge halafu taifa zima linabaki kumuomba mtu mmoja( rais) aingilie Kati suala hili ni uozo unaonuka.

Kungekuwepo na mifumo ama taasisi zenye nguvu zingerekebisha uozo huu
 
Bunge lenye wabunge fake, nalo Mambo yake mengi Ni fake
Aina ya wabuNge kama covid 19 inafanya kuwa vigumu kwa baadhi ya masomo shuleni mfano civics kufundishika,,kuna wakati ni vigumu kumfundisha mtoto aina za wabunge tulionao!
 
Naomba WANASHERIA wetu Waliobobea kwenye Masuala ya KATIBA watuelimishe KISHERIA Je Uwepo wa WABUNGE kinyume na KATIBA ya NCHI na Kushiriki VIKAO na Kuchangia HOJA Mbalimbali na Kupitisha Misuada na SHERIA mbalimbali huku Wakiwa Hawana SIFA za kuwa WABUNGE Kutokana na KUFUKUZWA Uanachama Wao ndani ya CHAMA Chao Je BUNGE hilo ni HALALI kwa MUJIBU wa SHERIA?
Bado bunge letu ni joke. Sincerely Unawezaje kuwa na mtunga sheria std 7 kwa mfano!
 
huku Wakiwa Hawana SIFA za kuwa WABUNGE Kutokana na KUFUKUZWA Uanachama Wao ndani ya CHAMA Chao Je BUNGE hilo ni HALALI kwa MUJIBU wa SHERIA?
1. Hapana SI HALALI . Ni kutokana na KUTOCHAGULIWA NA CHAMA CHAO KUINGIA BUNGENI kabla hata hujaongelea KUFUKUZWA!

2. Bunge NI HALALI ; lakini Vikao vya Bunge vinakuwa BATIRI maana vimejumuisha wasio Wajumbe halali! Mbaya zaidi ni kuwa tunaendelea kuwa na Bunge lenye SPIKA NA NAIBU WAKE WAVUNJA KANUNI ZA KUDUMU ZA BUNGE
 
Wakati wa Magu Chadema walijifanya washamalizana na Kina Mdee na hawawatambui, issue ya Bungen wakasema haiwahusu

Baada ya Mzee kufariki sasa wamerudi wanataka waondolewe kwa kuwa si Wawakilishi wa Chadema


Sababu ya kukataa kupeleka Wawakilishi wao ni kutotambua Matokeo ya Uchaguzi Mkuu na Bunge kwa jumla lakin Wametambua Mamlaka ya Spika hadi wamemuandikia Barua
 
Jibu analo Ndugai na Tulia...mama SSH ana mtihani mgumu, maana Mwendazake alimwachia viporo kwenye mtihani mgumu.
 
Hongera sana maana kati ya mada zote zilizowahi kuibuliwa humu kuhusu utata wa wabunge hawa, hakuna inayoibua mjadala mzuri kama hii uliyoianzisha wewe.

Ni kweli ni lazima tujiulize swali hili, kuwa;

Kama wabunge hawa siyo halali kikatiba lakini wakati huohuo wanashiriki kupitisha maamuzi mbalimbali ndani ya binge zikiwemo sheria, maazimio nk.

Hayo yanayopitishwa yanapata vipi uhalali wa kisheria iwapo kuna wasio halali kisheria kuyapitisha?

Huu ni majadala muhimu sana kwa watu wenye ufahamu tu. Nashauri wasiofikiri vizuri na wapenda mipasho wakae pembeni, wasiharibu mjadala huu.
 
Naomba WANASHERIA wetu Waliobobea kwenye Masuala ya KATIBA watuelimishe KISHERIA Je Uwepo wa WABUNGE kinyume na KATIBA ya NCHI na Kushiriki VIKAO na Kuchangia HOJA Mbalimbali na Kupitisha Misuada na SHERIA mbalimbali huku Wakiwa Hawana SIFA za kuwa WABUNGE Kutokana na KUFUKUZWA Uanachama Wao ndani ya CHAMA Chao Je BUNGE hilo ni HALALI kwa MUJIBU wa SHERIA?
Hawa Wabunge 19 watamtafuna Mr. Mnyika hadi ale wembe. Kuna barua yake kamili Tume ya Uchaguzi inayotoa hayo majina passport shaka, kwa nini anaulizwa Spika?

Kilichotokea ni kwamba kamati kuu walitaka waingie wake zao na Mrs Lissu, ikawa too late bana. CHADEMA hawatomsaheme Mnyika kwa hili, angesubiri kidooogo!

Ikumbukwe pia kuna rufaa ilipokelewa wakaahidi watajibu but we have waited and waited but where! Pia kuna Mawakili nguli fatmakarume na tundulissu wako tayari kuwatengenezea plaint (ingawa she personally cannot appear in court kumbe alimtukana Jaji Feleshi), hiyo nayo hawataki.

Sasa kaachiwa huyu Mpogoro Mrs Kiwanga wa Kiswahili kigumu anafanya mapress conference toxic, lakini kwenye uchaguzi majuzi akabwagwa chini puu!
 
Linakuwa halina tofauti na mkutano wa hadhara wa kijiji...
Weeee, wacha hizo! TLS haijafa bwana, it is alive and kicking. Umesahau majuzi tu Dr Kamelezya ndiyo sijui mkuu wao alimwagiza Samia (hazarani) aitishe uchaguzi mpya ili apate mbunge awe Waziri Mkuu aape kwake upya?

Hiyo wengi hatukulielewa, I daresay hata marais wastaafu tundulissu na fatmakarume wakazeleu. Ikajaishia kwa Ng'wiguluchemba kumwambia arudi shule. Bila hivyo baada ya muda wangeanza kusema serkali haina Waziri Mkuu.
 
Back
Top Bottom