Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Kusuhu hali ya Ugonjwa wa Figo nchini
Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel, amezungumzia ongezeko la magonjwa ya figo nchini, akitaja vichocheo vikuu vinavyosababisha hali hii kuwa mbaya. Akizungumza Bungeni leo Dkt. Mollel amesema kuwa sababu za msingi zinazochangia kuumwa kwa magonjwa ya figo ni pamoja na shinikizo la damu, kisukari, matumizi holela ya dawa, matumizi ya vilevi, na tumbaku.
Mbunge wa Viti Maalum (CHADEMA) Halima Mdee ameiuliza Serikali kuwa lini itaanza msako wa kuondoa pombe kali zenye sumu zinazouzwa kwa bei nafuu ambazo zinachangia ongezeko la magonjwa ya figo kwa vijana nchini.
Swali hilo limeulizwa Bungeni Jijini Dodoma na kujibiwa na Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel ambaye ameeleza kuwa Serikali itafanyia kazi wazo hilo.
Kuhusu gharama za kuunganisha Umeme
Mbunge wa Konde (ACT Wazalendo), Mohammed Issa, ameishauri serikali kufuta gharama za kuunganishwa na umeme (connection fee) kwa wananchi wote, bila kujali maeneo wanayoishi, akisisitiza kuwa wapo watu wenye kipato cha chini mijini na vijijini ambao wanashindwa kumudu gharama hizo.
Akichangia Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa mwaka 2025/2026, Issa ameeleza kuwa mipango ya sasa ina upendeleo kwa wakazi wa mijini kutokana na gharama za kuunganishwa na umeme kuwa ndogo ukilinganisha na vijijini, ambako mara nyingi kunahitajika nguzo nyingi na hivyo kuongeza gharama kwa wananchi.
"Kwenye suala la connection ya umeme... siku zote nimekuwa nikichangia suala la umeme kutenganisha mijini na vijijini bila connection fee," amesema Issa na kuongeza, "Mimi si muumini nalo kwa sababu wananchi hata kule mjini kuna maskini wengi na hawana uwezo lakini hata connection kwa sehemu za mijini ni rahisi lakini vijijini lazima unapata nguzo mbili, tatu gharama ni kubwa."
Pia, soma: Bunge la 12 Mkutano wa 17 Kikao cha Tano Novemba 4, 2024