Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Bunge linapokea na kushauri kuhusu mapendekezo ya mpango wa maendeleo unaokusudiwa kutekelezwa na serikali kwa Mwaka wa Fedha 2025/26. Majadiliano yanaendelea…
Shamsi Vuai Nahodha: Nitaongea hoja nne kuhusu mapendekezo ya mpango wa maendeleo wa taifa. Mwaka 1969, Waziri Mkuu wa zamani wa Singapore alitembelea Ghana na alipokutana na mwenyeji wake alitambulishwa kwa msomi wa Shahada ya Uzamivu. Aliporudi Singapore alifanya mkutano na waandishi wa habari na kusema kama angepata nafasi ya kuzishauri nchi za Kiafrika, basi angezishauri ziwekeze kikamilifu katika sekta za kilimo kwasababu kilimo ndiyo sekta yenye uwezo wa kuondoa umasikini katika bara la Afrika.
Maneno hayo hayo, Mwalimu Nyerere aliyarudia mwaka 1985 wakati akihutubia Mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM.
Hoja yangu ya kwanza, Kilimo kitaendelea kuwa na mchango mkubwa sana katika maendeleo ya taifa hili kwa miaka mingi ijayo. Na sekta hii inaajiri zaidi ya 70% ya Watanzania. Kama tunataka tupunguze umasikini miongoni mwa Watanzania, basi tuwekeze katika sekta ya kilimo. Sasa nieleze tu namna Wizara ya Kilimo inavyotekeleza miradi yake ya maendeleo.
Wizara hii inatekeleza miradi miwili ya kilimo – mradi wa Jenga Kesho iliyo Bora na ujenzi wa mabwawa 18 ya kilimo cha umwagiliaji. Nimezitafuta takwimu ili nione namna mradi wa Jenga Kesho iliyo Bora unavyoweza kutusaidia kukuza kilimo. Taarifa hizo sikuzipata. Katika mradi wa mabwawa 18, mpaka sasa kwa kipindi cha miaka mitatu wizara imetekeleza mabwawa matatu na mengine 15 yapo katika hatua mbalimbali.
Kwa busara za kawaida, Wizara ilitakiwa kutekeleza mabwawa manne kila mwaka badala ya kujenga mabwawa yote kwa wakati mmoja kama wanavyofanya. Kama wangefanya hivyo, leo ungekuta wamejenga mabwawa 12 na mabwawa sita yaliyobaki yangemalizwa mwaka kesho.
Hoja ya pili, licha ya wizara hii kupatiwa trilioni kila mwaka kwa ajili ya maendeleo ya kilimo, tija katika uzalishaji wa mazao ya kilimo bado upo chini sana.Nitatoa takwimu kuonesha namna gani majirani zetu wanapiga hatua kwenye sekta hii kuliko sisi.
Nchi moja ya jirani ina eneo la umwagiliaji lenye ukubwa wa hekta 650,000 na wanauza mazao ya kilimo nje ya nchi yenye thamani ya dola bilioni 3.2. Sisi Tanzania tuna eneo la kumwagilia lenye ukubwa wa hekta 827,000 na tunauza nje mazao ya kilimo yenye thamani ya dola bilioni 2.3. Utaona ni kwa jinsi gani tupo nyuma.
Nilitegemea fedha hizi za bajeti zingetumika kuwapa wakulima mbegu zilizo bora, huduma bora za ugani, utafiti wenye matokeo sahiji kwa wakulima, lakini hili nalo halikufanyika kwa usahihi.
Hoja ya tatu, njia muafakla ya kuongeza tija katika uzalishaji, iwe ni katika sekta ya kilimo au au sekta ya viwanda, ni kuwekeza kwenye elimu bora inayosisitiza ufundi, ujuzi na ugunduzi. Kwa bahati mbaya, elimu yetu bado haikidhi kiwango hicho cha ubora na mara nyingi tunafundisha masomo ya jumla jumla badala ya masomo yanayosisitiza ujuzi, weledi na umahiri.
Tunatumia wastani wa bilioni 500 kila mwaka kwa ajili ya mikopo ya elimu ya juu, lakini fedha hizo mchango wake ni mdogo. Ningepenfekeza masomo kama vile usimamizi wa mipango, usimamizi wa rasinimali, usimamizi wa viwanda na sekta ya afya. Mambo ambayo yana uhusiano wa moja kwa moja mna kupunguza umasikini.
Vilevile tungefundisha masomo ya ukalimani na Kiswahili kama lugha ya kigeni ili tusafirishe wataalamu nchi za ughaibuni. Kwenye teknolojia nilitarajia tungewafundisha vijana masuala ya sayansi ya data (data science), data analytics, akili bandia (AI), cyber na blockchain.
Hoja ya nne, baadhi ya matumizi ya serikali, kwa maoni yangu, badala ya kusaidia kuongeza tija, yanaibebesha serikali mzigo mkubwa sana. Mfano, Wizara za Mifugo, Kilimo Maliasili, na ya Maji wananunua mitambo inayofanana na wote wanafanya kazi za kuchimba mabwawa pamoja na kutengeneza barabara, Baada ya muda mfupi tu, vifaa vianaanza kutelekezwa porini kwakuwa gharama za mafuta na matengenezo zimekuwa kubwa sana. Napendekeza vifaa hivyo viweke sehemu moja na kila mmoja akodi.
Chuo Kikuu cha Daodoma kina shule nzima ya Teknolojia ya Habari, wakati huohuo, Wizara ya Habari inajenga Chuo cha Umahiri wa TEHAMA. Kwangu mimi hay ani matumizi mabaya sana ya fedha. Tatizo letu kama taifa si majengo, tatizo letu ni walimu walio bora, vifaa vilivyo bora, mazingira bora. Sasa, fedha zinazotumika kujenga chuo zingepelekwa Dodoma.
Prof. Shukrani Elisha Manya: Waziri alisema furaha ya wananchi imeongezeka baada ya serikali yao kukamilisha miradi mikubwa ya SGR, yeye alisema DP-World, lakini mimi naomba niweke na Bwawa la Nyerere. Mh. M/kiti, ni kweli kwa wale ambao wamesafiri na SGR wote wanafurahia maamuzi na utashi wa utekelezaji wa serikali yao wa kufanikisha miradi mikubwa. Na kwa jinsi hiyo, ni kweli kwamba kumbe serikali ikiamua, ikapanga vyema, inaweza kufanya na kuongeza furaha ya wananchi. Na kwakweli kwa hili, serikali heko sana!
Hii ni kwasababu SGR imerahisisha usafirishaji. Kila mtu sasa anatamani kusafiri kwa SGR apunguze masaa mengi ya kusafiri toka Dodoma kuja Dar es Salaam na tunaiomba serikali vile vipande vya kutokea Dodoma kuelekea Mwanza na vyenyewe vifanywe haraka kwa umahiri huohuo.
Bwawa la Nyerere limepunguza migao ya umeme na hivyo limeongeza furaha ya Watanzania. Furaha ya Watanzania itakuwa maradufu endapo miradia mambayo imekuwa ikitajwa mwaka hadi mwaka na yenyewe ikatekelezwa mapema kwa kadiri inavyowezekana. Mfano Mradi wa LNG )mradi wa kusindika na kuchakata gesi). Mradi huu ukianza mapema ni kichocheo cha viwamnda vya mbolea, kemikali nav yote ambavyo tukiongea BRT tunaagiza mbolea nje. Tuta-save pesa tunayotumia kuagiza mbolea.
Mwingine ni Mradi wa Chuma Leganga. Mradi huu umekuwa ukihuishwa katika hotuba za bajeti za serikali kila mwaka. Tunatengeneza reli kwa kutumia chuma nyingi sana. Ingekuwa habari gani kama tungetumia chuma chetu wenyewe.
Majadiliano yamekuwa yanachukuwa mda mrefu. Tuweke ukomo. Mimi ningetamani ili tuweze kupata manufaa ya kazi na miradi mikubwa inayoendelea, vihatarishi tuangalie kwamba majadiliano yafanywe kuwa mafupi ili ifikie mahali miradi hii ianze.
Lakini pia, kwakuwa tunaongea masuala ya bajeti na kubana matumizi, lazima tunapofanya majadiliano ya mambo haya makubwa mfano LNG na taasisi za kimataifa, tuzingatie watu wawekeze katika weledi mkubwa katika majadiliano ili serikali isiendelee kupoteza fedha za kutoingia kwenye mikataba ambayo ni ya maslahi kwa taifa. Tumeendelea kulipa mabilioni kwasababu ya mikataba.
Moja ya mambo muhimu katika utekelezaji wa bajeti ni suala la kubana matumizi ya fedha za uendeshaji na badaka yake kuwekeza fedha nyingi katika shughuli za maendeleo. Lakini pia ni kuwepo kwa utendaji wa pamoja baina ya wizara kwa wizara na taasisi kwa taasisi za serikali. Hili hjambo mwisho wake ni huduma bora kwa wananchi.
Dkt. Charles Kimei: Ukiangalia maandikoutagundua uchumi wa Dunia na Tanzania unaelekea uelekeo tofauti na tulipotoka wakati wa UVIKO-19. Utaona mfumuko wa bei duniani pia umepungua kutoka 8.1% kufikia 5.9% katika kipindi cha mwaka huu tulio nao.
Maendeleo haya yanatupa fursa nyingi. Kwa mfano, nchi zilizoendelea, mfano Marekani, zilianza sera ya kubana money supply (ujazo wa fedha) kwa kuongeza riba mara tu inflation ilivyokuwa imekuwa juu sana. Sasa imeshuka, ilikuwa kwenye two digits na sasa imefika 5.9%. Nchcji ya Marekani inaelekea kurekebisha sera ya kubana na hivyo riba zitashuka na tutaweza kukopa kwa gharama nafuu sana.
Kenye nchi za EAC na SADC, inflation imepanda sana. Kuna nchi kama vile Burundi imefikia takribani asilimia 20, ukienda Sudan Kusini ni 40.2, na ukienda kwenye nchi nyingine ni vivyo hivyo ukilingani na inflation ya nchi yetu ambayo ni 3%. Sisi tuna reserve ya chakula NFRI na tutawawezesha wananchi wetu kuuza chakula kule.
Maswali na majibu
Prof. Kitila Mkumbo: Serikali imeendelea kutekeleza miradi ya kimkakati katika Wilaya ya Tunduru. Miradi ya elimu inayotekelezwa inajumuisha ujenzi wa vyumba vya madarasa, bweni kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum, nyumba za walimu, shule mpya, kituo cha walimu, maabara, na ukarabati wa mabweni na shule kongwe.
Kwa upande wa afya, Serikali imeendelea na ukarabati wa hospitali ya wilaya, ujenzi wa vituo vya afya, jengo la dharura, nyumba za watumishi, ukamilishaji wa zahanati, na wodi mbili za wazazi. Katika sekta ya uchumi, Serikali inajenga soko la madini ili kuimarisha shughuli za kiuchumi wilayani humo.
Viongozi wa Wilaya ya Tunduru kuendeleza ubunifu katika kuanzisha miradi mingine ya kimkakati ya kiuchumi, kwa kushirikiana na sekta binafsi kupitia ubia mbalimbali, ili kuchochea maendeleo ya wananchi wa Tunduru.
Charles Mwijage: Serikali haijachukua hatua za kutosha kuweka mazingira yanayotosheleza kuendeleza soko la samaki nchini Tanzania. Sekta hiyo imekuwa chanzo cha aibu kwa taifa, kwani Tanzania haijaingia katika orodha ya nchi zinazofanya ufugaji wa samaki barani Afrika, licha ya rasilimali ya maji mengi inayopatikana nchini.
Hatujafanya lolote, hatujatumia maji yetu, hakuna chochote kimefanyika, tunachezea maji,” amesisitiza Mwijage. Morocco wanapata Dola Bilioni Moja kutokana na samaki. Misri anatuongoza...
Dk Godwin Mollel: Wizara ya Afya inatarajia kuanzisha Programu ya Taifa ya Lishe pamoja na kuanzisha kitengo cha utafiti wa lishe katika Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR). Hivyo, yale majukumu yaliyokuwa yanatekelezwa na TFNC yatafanyika kwa upana wake na Programu ya Taifa ya Lishe.