Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Wakuu
Baada ya mapumziko ya mwisho wa wiki, leo mkutano wa 18 wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, katika kikao chake cha 10 linaendelea ambapo baada ya Kipindi cha Maswali na Majibu itakuwa ni zamu ya kamati nyingine mbili za kudumu za Bunge kuwasilisha taarifa zao kwa kipindi cha kuanzia Februari 2024 hadi Januari 2025.
Kamati hizo ni ile ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) na Kamati ya Bajeti.
Kwa mujibu wa ratiba ya leo, baadhi ya wizara zitakazoulizwa maswali ni Ofisi ya Waziri Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) ambayo huwa haikosi maswali, Ofisi ya Rais (Mipango na Uwekezaji), Wizara ya Nishati, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi na nyinginezo.
Prof. Kitila Mkumbo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji
"Yale mashirika ya umma ambayo tumesema yafanye biashara, yafanye biashara kweli bila kuingizia serikali gharama yoyote, lakini tusingetaka kuona mashirika ya umma yashindane na Sekta Binafsi. Tumeshakubaliana kwamba muhimili wa uchumi wa nchi hii ni uimara ya sekta binafsi."
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Daniel Sillo, amesema Serikali itaendelea kuchangia fedha kukamilisha ujenzi wa vituo vya polisi nchini vinavyojengwa kwa nguvu za wananchi ili kuunga mkono juhudi zao.
Amesema tayari Serikali imetoa shilingi 236,408,000 kwa ajili ya kukamilisha vituo vya polisi Kambikatoto, Makongolos, Sangambi, na Igulusi mkoani Mbeya.
Kwa vituo vya Kandete, Itumbi, Igoma, na Madibira, amesema tathmini imekamilika, ikibainika kuwa zinahitajika shilingi 1,429,000,000, na maombi ya fedha hizo yamewasilishwa Makao Makuu ya Jeshi la Polisi.
Aidha, amesema ujenzi wa Kituo cha Polisi Kapunga unaendelea kwa ufadhili wa mwekezaji wa shamba la mpunga, huku Kituo cha Ifumbo kikijengwa kwa ufadhili wa mwekezaji wa madini wilayani Chunya.
Naibu Waziri alitoa kauli hiyo wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu, Suma Fyandomo, aliyetaka kujua lini Serikali itakamilisha ujenzi wa vituo hivyo mkoani Mbeya.
Serikali Kuboresha Biashara ya Tanzanite
Mbunge wa Arusha Mjini, Mrisho Gambo, amehoji lini Serikali itaruhusu uuzaji wa Tanzanite katika masoko ya ndani.
Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Stephen Kiruswa, amesema marekebisho ya kanuni ya Eneo Tengefu la Mirerani (2019) yameruhusu uuzaji wa Tanzanite ghafi nje ya Mirerani kwa wenye leseni kubwa ya ukataji, huku iliyokatwa na kung’arishwa ikiuzwa kwa yeyote mwenye leseni ya biashara au ukataji.
Kwa mwaka wa fedha 2024/2025, Serikali imepanga minada na maonyesho ya madini katika Arusha, Mirerani, Mahenge, Dar es Salaam, na Zanzibar, huku mnada wa kwanza ukifanyika Mirerani, Desemba 14, 2024.
Mbunge ashauri SGR iwe na matangazo mengine siyo royal tour pekee
Mbunge wa Nkasi Kaskazini, Aida Khenan, ameishauri Serikali kuboresha huduma za SGR kwa kutumia matangazo ya biashara kama chanzo cha mapato.
Ameshauri pia kuboresha miundombinu ya treni za mizigo na kufunga kamera kudhibiti hujuma. Ametoa ushauri huo Februari 10, 2025, Bungeni Dodoma, akichangia hoja za Kamati za PIC na Bajeti.
Bunge lataka serikali iondoe ruzuku kwa mashirika yanayojiendesha kibiashara
Bunge limeazimia serikali kuondoa ruzuku kwa mashirika yanayojiendesha kibiashara ili yaweze kujiendesha kibiashara, kukidhi bajeti zao na kutoa gawio kwa serikali.
"Baadhi ya Mashirika ya Umma yanayojiendesha kibiashara na yalitakiwa kujitegemea bado yanapata ruzuku kutoka Serikali Kuu"
Kiwango cha uhimilivu PSSSF kipo chini
Kamati ya Bunge ya Bajeti imesema kiwango cha uhimilivu cha Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) ni asilimia 36.4, chini ya kiwango kinachokubalika cha asilimia 60 na lengo la chini la asilimia 40.
Mwenyekiti wa kamati hiyo, Oran Njeza, akiwasilisha taarifa ya mwaka bungeni leo, amesema mifuko ya hifadhi ya jamii inafanya uwekezaji usio na tija. Kwa miaka ya fedha 2021/22 na 2022/23, PSSSF imelipa mafao ya Sh. trilioni 4.34 huku ikipata faida ya Sh. trilioni 1.8, ikionyesha uwiano usio mzuri kati ya malipo na mapato yake.
Bunge limeazimia kwamba serikali ihakikishe mifuko ya hifadhi ya jamii inasimamiwa ipasavyo ili kuhakikisha uwekezaji unakuwa wa tija, kupunguza vihatarishi na kuwezesha malipo ya mafao kufanyika kwa wakati.