Bunge la 12 Mkutano wa 18 Kikao cha 12 Februari 12, 2025

Bunge la 12 Mkutano wa 18 Kikao cha 12 Februari 12, 2025

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Leo katika kikao cha 12 cha mkutano wa 18, Bunge linajadili Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Usimamizi wa Mazingira wa 2024, ambapo Waziri wa Nchi (Muungano na Mazingira) atatoa maelezo.

Pia, Mwenyekiti wa Kamati ya PAC atawasilisha taarifa ya shughuli za kamati hiyo kwa mwaka 2024 kwa mjadala na maamuzi.

Katika Kipindi cha Maswali na Majibu, wizara mbalimbali zitajibu jumla ya maswali 19 ya msingi, ikiwemo TAMISEMI, Nishati, Afya, Kilimo, Uchukuzi na Fedha.



PAC yabaini kasoro ujenzi Uwanja wa Ndege wa Msalato

Kamati ya Bunge ya PAC imegundua dosari katika ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Msalato, ikiwemo ajira kwa wahandisi wasiosajiliwa, ujenzi bila vibali, ongezeko la gharama kwa Shilingi Bilioni 3.04, na ucheleweshaji wa malipo ya mkandarasi hadi Shilingi Bilioni 5.729. PAC imetaka serikali kuhakikisha miradi inatekelezwa kwa kufuata sheria ili kuepuka upotevu wa fedha za umma.
 
Mkuu nakupongeza sana kwa kutuletea habari za Bunge, ila hilo bunge limedharauliwa kabisa na wananchi.

Ndio maana hizi nyuzi hazina wachangiaji
 
Halina tija kwa taifa zaidi ya kututia hasara kwa kuteketeza kodi zetu kwa kulipana posho!
 
Tanganyika hainaga Bunge, tusidanganyane. Hivyo ni vikao vya kakikundi ka watu wachache kuifilisi nchi kwa maslahi yao.
 
Back
Top Bottom