Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Wakuu
Baada ya Kipindi cha Maswali na Majibu leo Februari 14, 2023, wabunge watajadili maelezo ya Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba kuhusu nyongeza ya bajeti na Muhtasari wa Tamko la Sera ya Fedha kwa mwaka 2024/2025.
Pia, kutakuwa na maswali 16 kwa wizara mbalimbali, mjadala wa hoja ya nyongeza ya bajeti, na usomaji wa kwanza wa miswada mitatu ya serikali:
1. Muswada wa Marekebisho ya Sheria Mbalimbali (2025).
2. Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya.
3. Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Shirika la Nyumba la Taifa (2025).
Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba apendekeza nyongeza ya TSh bilioni 945.7 kwenye Bajeti Kuu ya Serikali ya 2024/25 kutoka kwenye ile ya awali ya Trilioni 49.3 iliyowasilisha Bungeni Juni 13,2024.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji Prof. Kitila Mkumbo ajibu sakata la Bandari ya Bagamoyo. Asema Serikali haijaingia makubaliano yoyote ya uwekezaji
"Serikali ipo katika hatua mbalimbali za kutekeleza program ya ujenzi wa eneo maalum la kiuchumi la eneo la Bagamoyo na hili ni moja ya miradi 17 ya kielelezo iliyopo katika mpango wa tatu wa maendeleo ya miaka mitano 2021/22-2025/26"
"Pamoja na mambo mengine eneo hili linahusisha ujenzi wa miradi mingi lakini moja ni ujenzi wa Bandari, Kongani za Viwanda, Kongani za TEHAMA, Ukanda huru wa biashara na kituo cha Reli. Kwahiyo sio mradi mmoja na ndio maana tunaita program"
"Utekelezaji wa program hii utatekelezwa na sekta binafsi kwakushirikiana na serikali kupitia mpango wa ubia katika sekta binafsi na sekta ya umma yaani Public–private partnership (PPP)"
"Wadau mbalimbali kutoka ndani na nje wameonyesha nia ya kuwekeza, wadau hawa wako katika hatua mbalimbali za mazungumza na taasisi husika. Serikali haijaingia makubaliano yoyote na mwekezaji yoyote kwasasa, wala hatuna mkataba na mwekezaji yoyote katika miradi ya Bagamoyo ikiwemo niliyoitaja wa Bandari"