Bunge la 12 Mkutano wa 18 Kikao cha 4 January 31, 2025

Bunge la 12 Mkutano wa 18 Kikao cha 4 January 31, 2025

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Fuatilia Bunge la 12 Mkutano wa 18 Kikao cha 4 January 31, 2025


Bunge limepitisha Muswada wa Marekebisho ya Sheria za Kazi namba 13 wa Mwaka 2024, ambapo sasa likizo ya uzazi kwa mwajiriwa ambaye atajifungua mtoto njiti, imejumuisha muda uliobaki wa kufikia wiki 40 za ujauzito, huku baba naye akipewa siku saba za kupumzika.

Shirikisho la Vyama Vya Wafanyakazi nchini (TUCTA) ni miongoni mwa wadau ambao wamekuwa wakipaza sauti zao kutaka kuongezwa muda wa likizo za waajiriwa hao, ili kuboresha ustawi wa watoto hao.

Marekebisho hayo yamewasilishwa leo Januari 31, 2024 na Waziri wa Madini, Anthony Mavunde kwa niaba ya Waziri Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Ridhiwani Kikwete.

Akiwasilisha muswada huo, Mavunde amesema awali ilipendekezwa muda wa wiki 36 kama ukomo wa muda wa mtoto kutimia baada ya kuzaliwa kabla ya muda.

Hata hivyo, amesema baada ya majadiliano na kamati, Serikali ilikubaliana na mapendekezo ya kuongezwa muda huo hadi kufikia wiki 40 na kuongeza muda wa likizo ya baba, ambaye atapata mtoto njiti kutoka siku tatu hadi siku saba.

Taasisi ya Doris Mollel ambao ni moja wa waanzilishi wa wazo hilo, pamoja na Mtandao wa Haki ya Afya ya Uzazi nchini wamepongeza suala hilo ambalo wamekuwa wakilipigania kwa muda mrefu.

Dkt. Godwin Mollel, Naibu Waziri wa Afya

"Suala la akina mama [wajawazito] na mambo mengine ya dharura tunatoa maelekezo mahususi kwa hospitali binafsi lakini pia za umma kwamba, mama na mtu yeyote wa dharura akija ni lazima kwanza apate huduma sio suala la kuulizwa fedha au kufanya nini, huduma kwanza fedha baadaye."

Pia, amewataka wananchi kuacha matumizi holela ya dawa za binadamu zikiwemo tembe za uzazi za dharura (P2), wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Dk Tea Ntala.

Dk Ntala alihoji Serikali ina mkakati gani wa kuhakikisha matumizi ya P2 yanaelezwa vizuri ili wasichana wasije kuathirika baadaye kwa kukosa watoto.

Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Jerry Silaa amesema wizara yake kwa kushirikiana na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi iko kwenye mchakato wa kuweka mikakati thabiti ili kudhibiti utapeli mitandaoni ambao umetajwa kupungua nchini kwa asilimia 19.

Azimio la Dar es Salaam kuhusu nishati litafungua milango ya ajira kwa vijana wa Tanzania na Afrika, amesema Mbunge wa Singida Magharibi, Elbariki Kingu. Akizungumzia makubaliano ya mkutano wa wakuu wa nchi za Afrika uliofanyika Januari 27-28, 2025, Kingu amesema mikataba ya kufikisha umeme kwa watu milioni 300 ifikapo 2030 itawawezesha vijana kupata ajira na kupunguza uhamaji wa vijijini kwenda mijini.

Mbunge wa Makambako Deo Sanga ameitaka Serikali kuwaongezea posho ya madiwani kutoka Sh350, 000 kwa mwezi hadi Sh500, 000.
 
Yaani nusu saa nzima, hii yangu ndio comment ya kwanza...


Hakika kuna shida mahali... Nadhani watanzania tuna wivu sana!!
 
Hahahah!! Kikao cha chama
KAZI ni kipimo cha UTU
 
Back
Top Bottom