Bunge la 12 Mkutano wa 18 Kikao cha 7 Februari 5, 2025

Bunge la 12 Mkutano wa 18 Kikao cha 7 Februari 5, 2025

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Wakuu

Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, katika kikao chake cha saba, mkutano wa 18, leo Februari 5, 2025, litapokea taarifa, maoni na maazimio kutoka kwa Kamati ya Utawala, Katiba na Sheria pamoja na Kamati ya Sheria Ndogo.

Hatua hiyo itakuja baada ya kumalizika kwa Kipindi cha Maswali na Majibu.



Kinachoendelea Bunge Leo:

Serikali imesitisha mpango wa kulivunja Shirika la Elimu Kibaha baada ya mapitio, na badala yake litaendelezwa ili kuimarisha lengo lake la kuondoa umaskini, ujinga na maradhi, amesema Naibu Waziri wa Tamisemi, Zainab Katimba, akijibu bungeni.

Mbunge wa Mlalo(CCM), Rashid Shangazi ameitaka Serikali kueleza fursa zitakazopatikana kwa Watanzania mmoja mmoja na vikundi kupitia fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) 2027 zitakazofanyika Kenya, Uganda na Tanzania.

Akijibu swali hilo,bungeni leo Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamis Mwinjuma amesema kupitia mashindano haya fursa mbalimbali zitapatikana zikiwemo ajira kupitia ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya michezo itakayotumika wakati wa mashindano hayo.

Ametaja fursa nyingine ni uuzaji wa vifaa vya ujenzi, kuongezeka kwa mapato katika biashara mbalimbali kutokana na matumizi kwa wageni na wadau watakaoingia nchini kushuhudia mashindano.

Naibu Waziri wa Nishati, Mhe Judith Kapinga amesema kuwa hadi kufikia Januari, 2025, Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA), imekamilisha upelekaji wa umeme kwenye vijiji vyote 12,318 nchini na kwamba kazi inayofanyika sasa ni kuendelea kusambaza umeme vitongojini.
 
Seroius unatuletea habari za bunge kama vile tunahitaji kuzujua!
 
Back
Top Bottom