Bunge la 12 Mkutano wa 18 Kikao cha 8 Februari 7, 2025

Bunge la 12 Mkutano wa 18 Kikao cha 8 Februari 7, 2025

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Katika kikao chake cha Nane (8), mkutano wa 18, leo Februari 7, 2025 wabunge watapokea, kusikiliza, kujadili na hatimaye kupitisha au kukataa taarifa za kamati mbili za kudumu za Bunge baada ya Kipindi cha Maswali na Majibu.

Kamati hizo ni ile ya Ardhi, Maliasili na Utalii pamoja na ya Maji na Mazingira kuhusu shughuli za kamati hizo kwa mwaka 2024.


Yaliyojiri leo Bungeni

Dkt. Festo John Dugange, Naibu Waziri TAMISEMI


"Mikopo ya asilimia 10 inatolewa kwa makundi maalum ya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu kupata mikopo isiyo na riba. [..] Aidha, umri wa ukomo katika mikopo kwa vijana umeongezwa kutoka miaka 35 hadi miaka 45."

Dkt. Godwin Mollel, Naibu Waziri wa Afya, amegiza Vituo vya Afya na Hospitali kuwa kusiwepo na Mtanzania yeyote atakayekosa huduma za afya kwa sababu ya kukosa fedha.

Serikali yapokea pendekezo la NEMC kuwa mamlaka kamili

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhandisi Hamad Yusuf Masauni, amesema Serikali imepokea na inaendelea kushughulikia mapendekezo matatu ya marekebisho ya Sheria ya Mazingira Sura 191.

"Tayari tumeandaa mpango kazi kabambe na hakuna kipengele kilichoachwa."

Miongoni mwa mapendekezo hayo ni kuifanya NEMC kuwa mamlaka, kutunga Sheria ya Uchumi wa Buluu, na kutambua Kituo cha Taifa cha Ufuatiliaji wa Kaboni (NCMC).
 
Nimemkubali amejibu kwamba wazee wasiende kujihakiki bali wabaki huko kwenye maeneo yao huko chini watafuatwa kwa ajili ya uhakiki
 
Back
Top Bottom